Ushirikiano
wa wananchi wote na wadau unahitajika katika kuhakikisha serikali inatimiza
jukumu lake la kulinda na kusimamia amani na uslama nchini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Evarista Kalalu
Kauli
hiyo imetolewa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alipokuwa
akichangia katika mkutano wa amani mkoa wa Iringa uliyoandaliwa na Jumuiya ya
waislamu wa Ahmadiyya na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa Siasa ni Kilimo
mjini Iringa.
Wamoja
amesema “serikali inalojukumu la kuhakikisha kuwa amani na usalama kwa watu
wote, lakini katika kutekeleza hilo unahitajika ushirikiano wetu sote”. Amesema
kuwa wananchi na wadau wote hawana budi kushirikiana katika kuhakikisha kuwa
amani inadumishwa nchini. Amesema kuwa upendo ni nguzo mihumu katika kudumisha
amani. Amesema amani haiwezi kuwepo kama hakuna upendo, na kushauri kuwa
viongozi wote wajitahidi kuhubiri upendo ili kujihakikishia uendelevu wa amani.
Katika
mchango wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhan Mungi amesema
kuwaamani haiwezi kutafsiriwa kwa tafsiri moja pekee, bali inatafsiriwa kwa
sifa zake. Amezitaja sifa hizo kuwa ni ukosefu wa vurugu na migogoro. Sifa
nyingine amezitaja kuwa ni pamoja na ukosefu wa vurugu na uadui. Nyingine ni
ukosefu wa chuki na ugomvi.
Mungi
amesema kuwa amani ya kweli inazo tabia sinazoonekana. Amezitaja tabia hizo
kuwa ni kujali, kuheshimu, haki kwa watu wengine. Amesema kuwa tabia nyingine
ni ukarimu na uvumilivu kwa imani ya watu wengine.
Amesema
kuwa amani haishikiki bali ipo katika akili na roho na inapimika kwa kutokuwepo
kwa vurugu.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Iringa, Theresia Mahongo amesema kuwa amani ni kichocheo kikubwa
cha maendeleo nchini. Amesema kuwa ili jamii iweze kuwa na maendeleo ni lazima
watu na makundi yote waweze kutii mamlaka zilizopo kisheria kwa sababu mamlaka
zote zinatoka kwa Mungu.
Evarista
Kalalu amewataka wadau wote wa amani kujiuliza wamefanya nini katika
kuhakikisha amani iliyopo inadumu na kuwa endelevu. “Tanzania hatuna mahali pa
kukimbilia iwapo tutaamua kuvunja amani iliyopo. Wote wasio na amani
wanakimbilia kwetu, hivyo sisi tutakimbilia kwa nani?” alihoji Mkuu wa Wilaya
ya Mufindi.
Amesema kuwa ni ukweli usiofichika kuwa katika jamii tunayoishi
wapo watu wasiopenda amani hivyo ni jukumu letu kuwaripoti katika mamlaka
husika. “Si kila mtu anaweza kuchukua hatua, hivyo tunahitaji kuwalinda wale
wote wenye mamlaka za kuchukua hatua” alisisitiza Evarista.
=30=
No comments:
Post a Comment