Na. Mwandishi Maalum, Iringa
Hifadhi
ya taifa ya Ruaha inaathiriwa na changamoto ya kukauka kwa mto Ruaha mkuu jambo
linalohatarisha maisha ya wanyama na uendelevu wa hifadhi hiyo.
Kauli
hiyo ilitolewa na kaimu mkuu wa hifadhi ya Ruaha, Halima Kiwango alipokuwa
akiwasilisha taarifa ya hifadhi ya taifa ya Ruaha kwa wakuu wa mikoa ya nyanda
za juu kusini waliotembelea hifadhi hiyo na kufanya kikao cha pamoja cha
maandalizi ya Utalii Karibu Kusini hifadhini hapo.
Kiwango
alisema kuwa changamoto kwa uhifadhi ni kukauka kwa mto Ruaha mkuu jambo
linalohatarisha uhai wa wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.
Akiongelea
sababu za kukauka kwa mto Ruaha mkuu, Kiwango alizitaja kuwa ni kilimo cha
umwagiliaji mashamba makubwa na madogo ya mpunga katika bonde la mto Ruaha
mkuu. Sababu nyingine alizitaja kuwa ni ongezeko la mifugo katika bonde la
Usangu na watumia maji katika bonde hilo. Nyingine ni uvamizi wa wanyamapori
katika maeneo ya nje ya hifadhi na ujangili wa Tembo.
Kaimu
mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha alizitaja changamoto nyingine kuwa ni
barabara kuu kutoka Iringa hadi lango kuu la kuingia hifadhi ya Ruaha kutokuwa
ya kiwango cha lami inachangia idadi ndogo ya watalii wanaotembelea hifadhi
hiyo.
“Kutokuwa na lango la kuingilia
hifadhini upande wa Usangu kumekuwa kukisababisha watalii wengi kutokufika
katika hifadhi ya Ruaha. Changamoto nyingine ni hifadhi bado haijajulikana sana
kwa watalii wa nje na ndani” alisema Kiwango.
=30=
No comments:
Post a Comment