Na. Revocatus Kassimba, Songea
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amewaasa vijana waliohitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kuwa wazalendo na wenye kuipenda nchi yao ili waweze kuitumikia ili iweze kuwa na Maendeleo endelevu
Ametoa wito huo leo wakati akifunga mafunzo awali ya kijeshi yaliyojulikana kama Oparesheni miaka 50 ya Uhuru yalitolewa katika kikosi cha jeshi 842 Mlale JKT kilichopo wilaya ya Songea mkoa wa Ruvuma
Mwambungu amewapongeza Vijana hao kwa kuonyesha moyo wa uzalendo toka wajiunge na mafunzo hayo hapo mwaka jana julai ambapo wamejifunza mambo mengi yakiwepo stadi za kazi na mafunzo ya awali ya kijeshi
Aliongeza kusema mafunzo haya yatasaidia kujenga moyo wa kuipenda nchi hususan kipindi hiki ambapo maadili miongoni mwa Vijana yanaporomoka hivyo kwa kujiunga na jeshi la kujenga Taifa Vijana hupata Elimu na maarifa ya kujitegemea na hatimaye kuwa Vijana mahili katika Utendaji kazi
Alitumia pia fursa hiyo kuwapongeza Vijana wote walioshiriki katika operesheni ya kusomba mahindi kutoka kwa wakulima kipindi cha mwisho wa mwaka uliopita ili kunusuru mazao ya wakulima kuharibika
“Nawapongeza kwa umahili wenu kipindi cha oparesheni ya kusomba mahindi kutoka kwa wakulima kwani agizo nililotoa kwa makamanda wenu lilitekelezwa vyema” sasa wakulima wana nufaika na kazi mliyoifanya huo ndoi uzalendo alisisitiza mkuu wa Mkoa
Awali akitoa taarifa ya mafunzo kwa mkuu wa mkoa Kaimu kamanda kikosi cha 842 KJ Mlale Meja T S Mpupu alisema mafunzo hayo ya awali ya kijeshi yalianza tarehe 26 Julai 2011 na yanahitimishwa tarehe 20 Januari 2012 lakini yatendelea hadi kipindi cha mkataba wa miaka miwili kitakapoisha
Aliongeza kusema wakati wanaanza kulikuwa na Vijana wapatao 827 kutoka katika mikoa yote ya Tanzania na wanapohitimu leo ni Vijana 822 kati yao wavulana ni 671 na wasichana ni 152
Aliendelea kueleza kuwa Vijana watano hawakuhitimu mafunzo kutokana na watatu kufariki dunia kwa matatizo ya ugonjwa na wawili walitoroka mafunzoni
Aidha kwa upande wake mwakililishi wa Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa Luteni Kanali Malembo aliwakumbusha wahitimu hao juu ya kiapo walichoapa mbele ya mgeni rasmi kuwa wataeendeleza utii na kuitumikia nchi ya Tanzania kwa uaminifu,utii na uhodari siku zote
Alisema kuwa watakapotoka hapo(Mlale) watasambazwa katika makambi mengine nchini ili wakaendelee na mafunzo ya stadi za uzalishaji hadi kipindi cha miaka miwili kitakapoisha hivyo aliwasihi kuwa na nidhamu
“Nidhamu ni kitu cha msingi unapokuwa Ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa” alisema Luteni Kanali Malembo
Kikosi cha jeshi Mlale JKT kilianzishwa mwaka 1970 kikiwa na Malengo ya kuwalea Vijana kwa kuwapatia mafunzo na stadi za uzalishaji mali ili wahitimipo waeze Aidha kuajiliwa na serikali au wajitegemee katika kuendeleza Uchumi wao na taifa.
No comments:
Post a Comment