Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Serikali imedhamiria kuona mji wa
Iringa unakuwa na kuwa na maendeleo endelevu kwa ustawi wa kwa kuandaa mipango
shirikishi kwa wananchi.
Kauli hiyoimetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano
wa wadau wa maandalizi ya mpango kamambe wa mji wa Iringa (Iringa Master Plan) iliyosomwa
na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita.
Dkt. Ishengoma amesema “lengo kuu la
kuandaa mpango kamambe ni kuwezesha ukuaji wa mji ambao ni endelevu katika
Nyanja za kiafya, usalama, mpangilio mzuri, muonekano mzuri na ustawi wa
jamii”. Amesema kuwa katika kufanikisha mpango huo, ushirikishaji mipango
iliyopita na inayoendelea ya kisera katika ngazi mbalimbali za utendaji
utazingatiwa.
Mkuu wa Mkoa amesema kuwa mpango
kamambe husimamia uendeshaji wa mji kwa muda wa miaka 20. Amesema kuwa mpango
huo unaweza kufanyiwa mapitio baada ya miaka mitano (5). Akiongelea umuhimu wa
mpango amesema kuwa mpango hutoa mwongozo wa matumizi mbalimbali kwa ujumla
kulingana na mahitaji ya jamii husika. Ameyataja matumizi hayo kuwa ni makazi,
biashara, viwanda, kilimo, ufugaji na matumizi mengineyo.
Akiongelea Sheria ya Mipango Miji
namba 8 ya mwaka 2007 na Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria
nyinginezo, hifadhi ya mazingira husimamiwa na mamlaka ya upangaji kwa
kushirikiana na wadau wa mji husika.
=30=
No comments:
Post a Comment