Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
Iringa
Jumla
ya mikataba 18 imesainiwa na wazabuni walioshinda zabuni yenye thamani ya zaidi
ya shilingi bilioni 3 mkoani Iringa.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mratibu wa Wakala
wa Barabara za vijijini na mijini (TARURA) Mkoa
wa Iringa, Mhandisi Juma Wambura katika taarifa fupi ya TARURA iliyowasilikswa
kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hafla fupi ya utiaji saini
mikataba ya ujenzi wa barabara na vivuko baina ya TARURA na wakandarasi katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Iringa jana.
Mhandisi
Wambura alisema TARURA mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara ya
halmashauri zote za mkoa.
“Mhe. mkuu wa mkoa,
TARURA Mkoa wa Iringa ilitangaza miradi ya barabara ya halmashauri zote za
mkoa jumla ya zabuni 26 zenye thamani ya shilingi bilioni 6.5 ambayo leo
utaishuhudia mikataba 18 ikisainiwa na wazabuni walioshinda baada ya mchakato
mzima wa manunuzi kukamilika yenye thamani ya shilingi bilioni 3.56” alisema mhandisi Wambura. Alisema kuwa mikataba
minane itasainiwa baada ya taratibu za manunuzi kukamilika.
Mratibu
wa TARURA mkoa aliwaasa wazabuni hao kutekeleza miradi hiyo kwa weledi na
ufanisi mkubwa pasipo kuchelewesha kama utaratibu wa miaka ya nyuma ulivyokuwa.
“Aidha,
ninawakumbusha wazabuni kuacha mazoea ya kutekeleza kazi chini ya kiwango kwa
visingizio mbalimbali. TARURA haitamvumilia mkandarasi yeyote atakayezembea
katika utekelezaji wa miradi hii”
alisema mratibu wa TARURA. Aliwahakikishia wakandarasi kupata ushirikiano
unaostahili katika kutekeleza majukumu yao.
Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) ulianzishwa kwa
mujibu wa Sheria ya wakala za serikali sura 245 na kutangazwa katika Gazeti la
serikali Na. 211 la tarehe 12/05/2017.
=30=
No comments:
Post a Comment