Halmashauri
nchini zimeshauriwa kulipa kipaumbele suala la vifungashio katika mazao ya
nyuki ili kutoa taarifa sahihi kwa mlaji.
Ushauri
huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Immaculte
Senje alipokuwa alitoa tathmini yake juu ya changamoto wanazokabiliana nazo
katika kufikisha asali sokoni muda mfupi baada ya kutembelea mabanda ya
Halmashauri katika maonesho ya kitaifa ya mazao ya nyuki yajulikanayo kama ‘Dar
es Salaam Honey Exhibition’ yanayoendelea katika uwanja wa maonesho ya biashara
ya Mwl. Julius Nyerere, barabara ya kilwa.
Senje
amesema kuwa mabanda mengi aliyotembelea yanakabiliwa na changamoto ya
vifungashio. Amesema “nadhani umefika wakati kwa Halmashauri zetu kulipa uzito
suala la vifungashio katika mazao ya nyuki ili kuweza kuendana na uhalisia wa
soko”. Amesema umuhimu wa vifungashio katika mazao ya nyuki hasa asali,
unamuwezesha mlaji kupata taarifa kamili juu ya bidhaa anayoitumia na kiwango
cha ubora wake.
Afisa Uhusiano wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu, Al-Haji M. Batenga alipotembelea banda la Manispaa ya Iringa katika Maonesho ya Asali
Mjasiliamali
Msafiri Chengula kutoka kikundi cha Anamed chenye mizinga zaidi ya 200 katika
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa amesema kuwa changamoto wanayoipata ni uuzaji
asali kwa njia ya lejaleja, jambo linalowasababishia tatizo katika kuhifadhi
fedha na kuzipangia matumizi sababu fedha hizo hazikai. Amesema kuwa uchomaji
misiti umekuwa ukiathili sana utengenezaji wa asali sababu nyuki wamekuwa
wakikimbia au kuungua. Changamoto nyingine ameitaja kuwa ni tabia ya wizi wa
asali katika kipindi cha uvunaji ambacho kwa wilaya ya Iringa amekitaja kuwa ni
kati ya miezi ya Mei hadi Julai kutokana na ukame hali inayowalazimisha
walinaji kuhamia msituni wakati huo.
Changamoto
ya vifungashio pia linaikumba Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa mujibu wa
Afisa Misitu wa Msaidizi, Enock Changime, amesema “sehemu ya kuhifadhia asili
asali ili iweze kuingia sokoni kwa maana ya vifungashio ni tatizo kwa sababu
vifungshio vingi vinatoka nchi ya Kenya”.
Changime
amesema kuwa changomoto nyingine ni udogo wa mwamko wa jamii katika suala la
ufugaji nyuki. Amesema manispaa ya Iringa imekuwa ikihamasisha jamii kujiunga katika vikundi na kuvipa
mafunzo juu ya ufugaji nyuki sambamba na na misaada ya mizinga ya kuanzia
ufugaji huo.
Amesema
kutikana na changamoto ya uhaba wa wataalamu, Manispaa ya Iringa imekuwa
ikifanya kazi kwa karibu na sna na Halmashauri ya wilaya ya Iringa katika
kuunganisha nguvu ya rasilimali wataalamu ili kuweza kukuza sekta ya nyuki
katika halmashauri hizo.
Akiongelea
umuhimu wa vifungashio katika kukuza soko la bidhaa nchini, Kaimu Meneja wa
Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Wakala wa Vipimo nchini Irene John amesema
ili bidhaa iweze kutambulika ndani na nje ya nchi suala la vifungishio sahihi
ni muhimu sana. Amesema kuwa ni vema kuyapa uzito unaoshahili mambo muhimu ya
kuzingatia wakati wa ufungashaji bidhaa za mazao ya nyuki, ameyataja mambo hayo
kuwa ni masharti kuwa ni kuandika maelezo na kiasi cha ufungashaji. Mengine
ameyataja kuwa ni uzuiaji wa ufungashaji wenye udanganyifu na uthibiti wa
vipimo.
Maonesho
ya kitaifa ya mazao ya nyuki yalianza katika uwanja wa maonesho ya biashara wa
Mwl. Julius Nyerere tarehe 4-7 Oktoba, 2012 na yalitanguliwa na kongamano la
kitaifa la wadau wa sekya ya asali kutokana na agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mizengo Pinda.
=30=
No comments:
Post a Comment