Hospitali
ya Aga Khan Iringa imefunga mashine mpya ya kisasa ya Ultrasound iitwayo
Sonoace R5 iliyotengenezwa na kampuni ya Samsung Medison kwa lengo la kutoa
huduma bora za Ultrasound mkoani Iringa na maeneo ya jirani.
Mtaalamu wa kuendesha mashine ya
Ultrasound katika Hospitali ya Aga Khan Iringa
John Mwega akifanya uchunguzi muda mfupi baada ya kufungwa kwa mashine ya
kisasa ya Ultrasound Sonoace R5 jana.
Mashine ya kisasa ya Ultrasound Sonoace R5
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na gazeti la Uhuru, Mratibu wa huduma za matibabu
(PMC) kwa hospitali za Aga Khan, Saidu Beyai amesema kuwa hospitali ya Aga Khan
imeamua kufunga mashine hiyo kwa lengo la kuboresha huduma za uchunguzi kwa
wagonjwa wanaohitaji uchunguzi huo kwa njia ya Ultrasound. Amesema kuwa mashine
hiyo pia itaboresha uchunguzi wa ubora wa huduma hiyo na matokeo yake kwa
wanawake wajawazito kwa haraka na ubora unaokubalika.
Nae
mtaalamu wa uendeshaji wa mashine hiyo, John Mwega amesema kuwa mashien hiyo
italeta mapinduzi ya kimatibabu katika uchunguzi na matibabu kwa sababu mashine
hiyo inazo probu tatu tofauti na ile ya awali iliyokuwa ndogo na kuwa na probu
moja jambo lilikuwa likizuia uchunguzi wa baadhi ya magonjwa katika mwili wa
binadamu. Amesema kuwa tofauti na ile mashine ya awali, mashine hii mpya
itakuwa ikiwezesha uchunguzi wa matatizo ya ndani zaidi ya wanawake tofauti na
mashine ya awali iliyokuwa inatumika zaidi nje (juu ya tumbo la mwanamke).
Mwega
amesema kuwa mashine hii kubwa zaidi itasaidia hata matatizo ya mishipa ya damu
kuweza kuangaliwa vizuri tofauti na awali sambamba na ubora wa picha
zitakazopigwa.
Akielezea
umuhimu wa mashine hiyo katika kumsaidia daktari kumhudumia mgonjwa wake
vizuri, mtaalamu huyo wa uendeshaji mashine amesema “unapoweza kutambua ugongwa
mapema unaweza kumhudumia mgonjwa wako mapena na kwa haraka hivyo kuweza
kuhudumia wagonjwa wengi kwa haraka tofauti na ilivyokuwa awali”. Amesema
mashine hiyo mpya inaweza kufanya uchunguzi kwa ogani za mwili kwa wanaume na
wanawake.
Amesema
kuwa mashine hiyo ni mzuri zaidi kwa sababu inao uwezo mkubwa wa kuhifadhi
picha na taarifa za mgonjwa jambo linaloweza kumsaidia daktari kuweza kufanya
ulinganifu na kushauriana na madaktari wengine katika kupata ufanisi wa tiba.
Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuweza kufika katika hospitali hiyo kwa ajili
ya huduma hizo bora na za kisasa za Ultrasound.
Ikumbukwe
kuwa hospitali ya Aga Khan imekuwa ikipokea kati ya wagonjwa 10-25 kwa siku kwa
huduma za Ultrasound.
=30=
Picha IMG 7863 mashine
ya Ultrasound Sonoace R5 jana ikioa
majibu ya kipimo.
No comments:
Post a Comment