Waziri Kagasheki
Waziri
wa Maliasili na Utalii Mheshimiwa Khamis Suedi Kagasheki amewaruhusu
watu 292 ambao vibali vyao vilisitishwa mwezi Januari mwaka huu,
kutokana na utata uliojitokeza, kuendelea na uvunaji katika Shamba la
Sao Hill. Waziri Kagasheki ametoa ruhusa hiyo baada ya kujiridhisha
kuwa watu hao walipata vibali hivyo kwa kufuata taratibu za uvunaji.
Mheshimiwa
Kagasheki wakati alipotembelea Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa tarehe
25 na 26 Januari 2013 ili kusikiliza kero zilizopo Wilayani humo
kuhusiana na Shamba la miti la Sao Hill, aliahidi kufanyia kazi
baadhi ya masuala yaliyojitokeza.
Kuhusu
suala la vibali 292 vilivyotolewa katika msimu wa mwaka 2012/13 na
kusitishwa wakati wa ziara yake, Waziri Kagasheki amelifanyia kazi na
kubaini kuwa matatizo na changamoto zilizojitokeza zilitokana na
utendaji katika kipindi cha mpito, hususan mabadiliko ya utaratibu wa
utoaji vibali vya uvunaji.
Hivyo,
wadau hao 292 ambao hawana vibali rasmi vilivyochapishwa kutokana na
kutumika utaratibu wa zamani, wameruhusiwa kukamilisha taratibu na
kupewa vibali rasmi vya uvunaji.
Ruhusa
hii inawahusu wavunaji wote waliofuata taratibu zote za usajili,
ikiwa ni pamoja na kupata usajili na kulipia maduhuli na tozo
mbalimbali za Serikali ambavyo ndivyo vigezo muhimu vya kumfanya
mvunaji kufanya shughuli zake zinazohusiana na masuala yote ya
uvunaji.
Wizara
ya Maliasili na utalii inaendelea kufanyia kazi kero zote
zilizojitokeza wakati wa ziara hiyo Waziri na taarifa itaendelea
kutolewa kuhusu utekelezaji wake.
George
Matiko
MSEMAJI
WIZARA
YA MALIASILI NA UTALII
Tarehe
21 Februari, 2013
|
No comments:
Post a Comment