Na: Atley
Kuni - Afisa Habari Mkoa wa Mwanza.
Leo kubwa katika Mkoa
wa Mwanza tumepokea Ugeni wa Wadau wa mashirika ya Maendeleo kutoka (DPG),
Ambalo linajumuisha balozi zote zilizopo hapa nchini, Zikiwapo Jumuiya ya
Ulaya,Wakuu wa Mashirika ya Ufadhili, wa Maendeleo kama NDP, WB, AFDB, JICA
UNICEF.
Ujumbe huu umefika
Mkoani hapa na Kuonana na Vingozi wa Mkoa wa Mwanza, akiwapo Mhe. Mkuu wa Mkoa
wa Mwanza, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na
watendaji wengine wa Mkoa na Halmashauri za Wilaya na Wataalam wengine wa
taasisi za umma zilizopo katika Mkoa huu.
Katika ziara yao
hiyo, wamepata kusikia Speach kuhusu Masuala Mbali mbali ya maendeleo katika
Mkoa huu. Lengo la Ziara Hiyo ilikuwa Kutembelea na kuona jinsi Miradi
mbalimbali ya maendeleo inavyo tekelezwa, hivyo wametembelea Miradi mbali mbali
ya Maendeleo katika Mkoa huu ikiwapo, Mradi wa barabara za
Mawe, unao tekelezwa katika Mkoa huu hususan katika Halmashauri ya Jiji la
Mwanza.
Hata hivyo kwa
mujibu wa ratiba yao siku tarehe 23/4/2013, watafanya ziara katika Mkoa wa
Geita.
Kuhusu mambo mengine
Mwanza ni salama, Mvua zipo za wastani, na jua linawaka kwa Mbali.
No comments:
Post a Comment