Salamu za Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma (Mb.) katika mazishi ya CPL Osward Paulo Chaula amesema yafuatayo:
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma (Mb.) akitoa salamu za Mkoa wa Iringa
Wanajeshi wakitoa heshima zao kwa marehemu CPL. Osward Paulo Chaula
Kwa
masikitiko makubwa kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Iringa, napenda
kutoa poke kwa familia ya Paulo Chaula kwa kufiwa na kijana wetu askari
CPL.Osward Paulo Chaula, ambaye alikuwa akishiriki ulinzi wa amani
nchini Darfur, Sudan.
Tukio hilo lilitokea tarehe 13 Julai, 2013.
Mkoa
wa Iringa na Taifa kwa ujumla, tunakiri kwamba tumeondokewa na kijana
wetu shujaa, mzalendona mchapa kazi ambaye umauti umemkumba akiwa
kazini. askari huyu alikuwa tegemeo kubwa kwa Taifa letu la Tanznaia.
Tunaahidi tutayaenzi yale yote mazuri aliyotuachia watanzania.
kutokana
na tukio hilo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa pamoja na Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Kilolo zinatoa pole ya Tshs. 500,000/= kwa familia ya Paulo
Chaula.
=30=
MATUKIO KATIKA PICHA YA MAZISHI YA MWANAJESHI ALIYEFARIKI DARFUR NCHINI SUDAN
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt Christine G. Ishengoma (Mb.) akisaini kitabu cha wageni katika mazishi ya CPL.Osward Paulo Chaula
Baadhi ya waombolezaji wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Waombolezaji wakiomboleza kifo cha CPL.Osward Paulo Chaula
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiaga mwili wa marehemu
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Gerald Guninita akiaga mwili wa marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa akiaga mwili wa marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakibeba jeneza lenye mwili wamarehemu wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wanajeshi vijana wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula ukipelekwa makaburini
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiweka udongo katika kaburi alimolala marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bibi Scolastica Mlawi akiweka udongo katika kaburi alimolala marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Waombolezaji wakiomboleza kifo cha CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wa JWTZ wakiendelea na taratibu za kijeshi katika mazishi
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiweka Shada la ua katika kaburi alimolala marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akikabidhi rambirambi kwa familia ya marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
No comments:
Post a Comment