Na
Charles Amulike - Iringa
Timu ya kuvuta kamba (wanawake)
ya clabu ya RAS Iringa imeanza safari yake kuelekea mkoani Dodoma kushiriki
mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Idara Serikali, Mikoa na Wizara
(SHIMIWI) ikitarajia kurudi na kikombe.
Katibu wa Clabu ya SHIMIWI ya RAS IRINGA Neema Mwaipopo (kulia) akimueleza Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa maandalizi ya timu
Hayo yamesemwa na Katibu
wa SHIMIWI Katika Ofiis ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Neema Mwaipopo wakati wa kuiaga
timu hiyo tukio lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
wa Iringa.
Mwaipopo amesema kuwa timu
hiyo yenye juml;a ya wachezaji 15 inakwenda mjini Dodoma kushiriki mashindano
hayo ya SHIMIWI kwa kucheza na timu za ofisi za wakuu wa mikoa, wizara na
taasisi mbalimbali za serkali. Ameongeza kuwa timu hiyo imejiandaa vizuri na
kutarajia kurudi na ushindi wa kishindo.
Akiongelea changamoto
wakati wa maandalizi ya timu hiyo Nahodha wa timu hiyo, Agness Mlula amesema
kuwa wachezaji wengi walishindwa kuhudhuria mazoezi kutokana na wengi wao
kunyimwa ruhusa kazini. Amesema pamoja na changamoto hiyo, timu hiyo imejipanga
vizuri na wanatarajia kurudi na ushindi katika mashindano hayo.
Timu hiyo inatarajia
kurudi mkoani Iringa tarehe 6 Oktoba mwaka huu 2013 mara tu watakapomaliza
mashindano hayo.
=30=
No comments:
Post a Comment