Mkuu wa Mkoa wa Iringa akiongea na ujumbe wa wanazuoni kutoka Angola
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma
Mkuu wa Mkoa akiongea na Wafanyabiashara wakubwa wa Mkoa wa Iringa (hawapo pichani) kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu
Mkuu wa Mkoa akiongea na Wafanyabiashara wakubwa wa Mkoa wa Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa (katikati) muda mfupi kabla ya kufunga mafunzo
juu ya mbinu za kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja mahala pa kazi kwa
watumishi wa TANAPA kutoka hifadhi za kusini yaliyofanyika katika ukumbi wa
Neema Craft Manispaa ya Iringa. Kushoto ni Mratibu wa SPANEST, Godwell Meing'ataki na Risala Kabongo (kulia) Afisa Utalii -TANAPA Kanda ya Kusini
Mkuu wa Mkoa wa Iringa akisoma hotuba ya kufunga mafunzo
juu ya mbinu za kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja mahala pa kazi kwa
watumishi wa TANAPA kutoka hifadhi za kusini yaliyofanyika katika ukumbi wa
Neema Craft Manispaa ya Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Irinag, Dk.Christine Ishengoma mwenye nguo nyekundu katika picha ya pamoja na wanasena wa TANAPA kanda ya kusini
Makamu wa Rais wa Commercial Seeds Production, Chadjen Ucharattana akimuonesha mahindi Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma akiangalia mahindi ya njano toka kwa Makamu wa Rais wa Commercial Seeds Production, Chadjen Ucharattana
Mkuu wa Mkoa wa
Iringa, Dk.Christine Ishengoma (kulia) akitoa taarifa kwa Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) katika
kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Ujenzi baada ya kukagua
barabara ya Iringa-Dodoma (km 260)
Waziri wa Ujenzi, Dk. John Pombe Magufuli (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk.Christine Ishengoma (kulia) wakifuatilia hali ya mambo katika kikao cha majumuisho ya ziara ya Waziri wa Ujenzi baada ya kukagua barabara ya Iringa-Dodoma (km 260)
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Wamoja Ayubu (kushoto) akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu- Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Sihaba Nkinga (kulia) katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Katibu wa Kamati ya Itifaki, Ratiba, mapokezi na Malazi, Neema Mwaipopo (kulia) akichangia mada katika kikao cha maandalizi ya Sherehe za Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na Wiki ya Vijana Kitaifa
No comments:
Post a Comment