Monday, October 14, 2013

MAADHIMISHO YA KILELE CHA MWENGE WA UHURU NI UMOJA NA MSHIKAMANO




Serikali imekumbusha kuwa lengo la maadhimisho ya kilele cha mbio za mwenge wa uhuru, kumbukumbu ya baba wa Taifa na wiki ya vijana ni kukumubuka mawazo ya mwalimu Nyerere kuhuru uhuru na umoja wa Tanzania na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

                                      Rais Dk. Jakaya Kikwete akihutubia wananchi

                                                                Vijana wa Halaiki

                                                       Vijana wa Halaiki

Kauli hiyo imetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete katika hotuba yake kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Kumbukumbu ya Baba wa Taifa na wiki ya vijana kitaifa yaliyofanyika katika uwanja wa kumbukumbu ya Samora manispaa ya Iringa leo.


Rais Kikwete amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo pamoja na mambo mengine ni kumbukumbu ya baba wa Taifa Mwalimu Juliua Nyerere. Amesema “watanzania wanajikumbusha mawazo ya baba wa Taifa kuhuru umoja na mshikamano w anchi yetu na watu wake na muungano wa Tanganyika na Zanzibar”. Amesema kuwa mawazo na mafundisho ya Mwalimu Nyerere ni dira katika kuelekea katika upatikanaji wa katiba mpya. Amesema “hotuba zake na mafundisho yake yatatusaidia sana katika mchakato wa Katiba mpya. Naamini fikra za mwalimu na mitazamo yake bado ina maana sana hata leo hii”. “Napenda mabadiliko ila mabadiliko yatakayotupeleka mbele si kuturudisha nyuma” alisisitiza Rais Kikwete.


Akiongelea ujumbe wa Mwenge wa Uhuru mwaka 2013, Rais Kikwete ameutaja kuwa ni “Watanzania ni wamoja” wenye kaulimbiu tusigawanywe kwa misingi ya tofauti zetu za dini, itikadi, rangi na rasilimali. Amesema kuwa kaulimbiu hii inasisitiza juu ya umoja na mshikanamo wa Taifa. Amesmea kuwa kutokana na umoja huo, hali ya nchi ni shwali na watanzania wanaendelea kushirikiana vizuri bila kubaguana kwa aina yoyote. Amesema kuwa kwa msingi huo, waliotaka kutufarakanisha hawakufanikiwa.


Akiongelea amani na utulivu nchini, amesema kuwa amani inaweza kutoweka kutokana kutokana kutenda dhambi kubwa ya ubaguzi. Amesema kuwa bila amani watanzania hawawezi kuishi kwa furaha na raha na jamii haiwezi kufanya kazi za kujiletea maendeleo. Amesisitiza kuwa iwatu amani ya nchi itachezewa na kutoweka, hakuna atakayebaki salama. Amesema kuwa serikali yake itaendelea kujenga na kudumisha amani nchini. Amewataka wananchi wote kwa umoja wao kukemea kwa nguvu  vitendo vyote vya kuvunja amani au vinavyopelekea uvunjifu wa amani. 


Akiongelea mapambano dhidi ya ukimwi, Rais Kikwete amesema kuwa tokea ujonjwa wa ukimwi uingie nchini mwaka 1983, zaidi ya wananchi milioni 2 wamepoteza maisha. Aidha, amepongeza juhudi zinazofanywa za mapambano dhidi ya ukimwi.  Amesema kutokana na juhudi hizo hali ya kiwango cha maambukizi kimeshuka kitaifa hadi kufikia asilimia 5.1 kwama 2012. 


Akiongelea adhari za maambukizi ya ukimwi, Rais Kikwete amesema kuwa ujonjwa huo umeacha watoto yatima na wengine kukatisha masomo ili walee wadogo zao. Amesema sehemu nyingi wazee ambao kwa umri wao wanastahili kulelewa ndio wamechukua jukumu la kulea watoto ambao wameachwa na wazazi wao baada ya kufariki. 
 
                              Wananchi waliofurika katika Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru

                            Wananchi waliofurika katika Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru

Amesema kuwa Serikali yake kwa kushirikiana na wadau wengine itahakikisha kuwa vijana hao walioachwa wanapata elimu bora ambayo ni ufunguo wa maisha yao ili waishi vizuri na kupata fursa kama watoto wengine. Amesem pamoja na jitihada za kuteremsha maambukizi kitaifa hadi kufikia asilimia 5.1 bado asilimia hizo ni kubwa sana na serikali inataka isibaki hata asilimia 1. Amesema serikali inataka asiwepo hata mtanzania mmoja mwenye maambukizi.


Amesema kuwa serikali itaendelea kuhimiza wananchi kuacna ngono zembe kwa kuhamasisha na kuelimisha juu ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya ukimwi. Aidha, ametoa wito kwa wanaume nchini ambao hawajafanyiwa tohara kujitokeza na kufanyiwa tohara ili kupunguza athari za maambukizi ya ukimwi. Aidha, amesema kuwa tohara si tiketi ya kutokupata maambukizi. 

=30=

No comments:

Post a Comment