6 Disemba, 2013 - Saa 17:22
GMT
Mandela atazikwa tarehe 15 mwezi
Disemba
Wananchi wamejitokeza katika sehemu
nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Nelson Mandela
Mandela.
Mji wa Johannesburg umemiminika watu
waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii, familia na
marafiki wao.
Viongozi duniani pia wameendelea
kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.
Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo
jana Alhamisi saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa
Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto
wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.
Je uko Afrika Kusini? Unaweza
kututumia picha au video kuhusu yanayojiri huko na tutayaweka hapa kwenye
mtandao wetu. Tutumie picha au ujumbe wako wowote kupitia ukurasa wetu
waFacebookbbcswahili
Mandela alifariki nyumbani kwake
mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Na wewe pia unaweza kutuma ujumbe
wako kupitia ukurasa wetu wa Bofya Facebook ambao kisha nitauweka kwenye
mtandao wa Bofya bbcswahili
Rais wa Uganda Yoweri Museveni
amesema kuwa Mzee Mandela, miongoni mwa wengine kama Oliver Tambo, Govan Mbeki
na wengine, walijitlea maisha yao na ujana wao wote katika kupigania haki na
kuikomboa Afrika Kusini. Walijivunia kweli walichoamini na wakatekeleza. Sasa
ni jukumu letu na wadogo wetu kuendeleza kazi ya Mandela.''
Rais wa Malawi Joyce Banda,
"Wakati kama huu, sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea,
lakini ni huzuni kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa
kumpoteza kijana wa Afrika Dr.
Nelson Mandela kwasababu vita
alivyopigana sio tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji
wa aina yoyote dhidi ya binadamu.
Na ndio maana vijana, na wazee, wake
kwa waume, weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu
alivyopigania."
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi
Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Waziri mkuu wa India, Manmohan
Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani.
Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa
wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka
yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.
Katika ulimwengu uliogubikwa na
migawanyiko, amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana
mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."
@bbc.co.uk/swahili/habari/2013/12/131206_mandela_dunia_omboleza.shtml
No comments:
Post a Comment