Na
Mwandishi Maalum Mbeya
Nafasi
ya teknolojia na ushirikishaji wadau wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na
ushirika ni ufunguo wa mafanikio kwa mkulima nchini.
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika wa Halmashauri ya
Wilaya ya Iringa, Lucy Nyalu alipokuwa akielezea mafanikio ya Halmashauri yake
kuwa mshindi wa kwanza katika maonesho ya Nanenane Nyanda za juu Kusini mwaka
2015.
Nyalu
alisema “Halmashauri ya wilaya ya Iringa
imejikita katika mambo makuu mawili; mosi, ni teknolojia ya kilimo na pili ushirikishaji
wadau wa sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi na ushirika ili kushirikiana nasi
katika kumkomboa mkulima wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa na taifa kwa ujumla”.
Alisema kuwa ushindi wa kwanza katika maonesho ya mabanda ya Nanenane Nyanda za
juu Kusini mwaaka 2015 ulitokana na chachu ya teknolojia na wadau kwa umoja wao.
Aliongeza “maonesho ya Nanenane kwetu ni
suala mtambuka, linalohusisha Idara zote za Halmashauri ndiyo maana utaona kila
Idara ipo hapa kuonesha ushirikiano na ushirikishaji wa shughuli zinazofanyika
katika Halmashauri pamoja na uchache wa rasilimali uliopo.
Wataalam na wakulima
wetu wote wamekuja kufundisha yale yanayofanyika katika Halmashauri yetu kwa
ufanisi mkubwa, na kujifunza mambo mapya kwa lengo la kuboresha zaidi utendaji
kazi”.
Akiongelea
Halmashauri yake ilivyojipanga katika maonesho ya Nanenane mwaka 2016, Nyalu
alisema kuwa Halmashauri yake imejipanga vizuri zaidi kwa kuongeza matumizi ya
teknolojia katika sekta ya kilimo na ushirikishaji wadau. Teknolojia hizo
alizitaja kuwa ni hifadhi bora ya mazao kwa kutumia mifuko ya pics na vihenge
vya chuma, teknolojia ya kuvuna maji kwa kutumia sola kwa matumizi ya majumbani
na kumwagiliaji, teknolojia ya kufukuza ndege kwenye kilimo cha mpunga, teknolojia
ya usindikaji mboga kwa kutumia sola, teknolojia ya usindikaji ngozi na
wanafunzi wenye ulemavu wanaochapa kazi katika kompyuta kwa kutumia miguu.
Halmashauri
ya wilaya ya Iringa, inatarajia kutetea ushindi wa kwanza katika maonesho ya
Nanenane Kanda ya Nyanda za juu Kusini
kwa kushirikisha wadau wa John Deere, One Acre Fund, Rudi, Asas Tahea, Vista,
Clinton Foundation, SNV na Britain.
=30=
No comments:
Post a Comment