Na.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Wakina baba mkoani Iringa watakiwa
kushiriki kikamilifu katika makuzi na maendeleo ya watoto ili kujenga jamii
familia imara isiyokuwa na utapiamlo.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa
Iringa, Mheshimiwa Amina Masenza akipokuwa akizindua kampeni ya Mama Msosi Lishe
katika bustani ya Manispaa ya Iringa jana.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Amina Masenza alimpatia uji mtoto Pricila Mgaya katika uzinduzi wa Kampeni ya Mama Msosi Lishe |
Mheshimiwa Masenza alisema kuwa Serikali ya
awamu ya tano chini ya Rais Dr John Magufuli inatambua umuhimu na kuwekeza
katika masuala ya lishe nchini.
“Huo ni
mojawapo ya mkakati wa kufanikisha azma ya Serikali kufikia uchumi wa
kipato cha kati na viwanda ifikapo 2025. Baraza la Umoja wa Mataifa liliweka
azimio la kuwa kati ya mwaka 2016 hadi mwaka 2025 ni miaka ya kuchukua Hatua
katika kutekeleza masuala ya lishe”
alisema mheshimiwa Masenza.
Aliwataka wananchi wa mkoa wa Iringa kuunga mkono
juhudi zinazofanywa na Serikali katika kupambana na tatizo la utapiamlo.
Aidha, aliwataka
kina
baba kushiriki kikamilifu katika ufuatiliaji wa makuzi na maendeleo ya watoto
pasipo kuwaachia kina mama peke yao.
Alisema kuwa hiyo ni njia ya kukabiliana
na tatizo la utapiamlo mkoani Iringa. Njia nyingine aliitaja kuwa ni uandaaji
wa chakula vizuri kutokana na maeneo mengi huloweka mahindi muda mrefu na
kupoteza madini na vitamin. Aliongeza kuwa ulishaji wa watoto wadogo uzingatie
vyakula mchanganyiko, idadi ya milo na kiasi cha chakula cha kumpa mtoto
kulingana na umri kuanzia kipindi mtoto anapotimiza miezi 6 mpaka miaka miwili.
Vilevile, aliwataka kina mama wajawazito kuanza mapema kliniki ya uzazi ili
kupata huduma muhimu. Alizitaja huduma hizo muhimu kuwa ni kupata vidonge vya
kuongeza damu, kusaidia ukuaji bora wa mtoto, dawa za minyoo, kuzuia Malaria na
VVU.
Katika maelezo ya awali ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa,
yaliyotolewa na Katibu Tawala msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratibu, Nuhu
Mwasumilwe alisema kuwa changamoto
kubwa katika Mkoa wa Iringa ni uelewa mdogo katika jamii wa masuala ya lishe.
Changamoto hizo alizitaja kuwa ani uandaaji wa chakula hasa
ugali kwa kutumia mahindi yaliolowekwa kwa muda mrefu maarufu kama ‘kiverege’ husababisha madini na vitamini zote kupotea.
Changamoto
nyingine ni watoto wadogo kulishwa milo ya watu wazima isiyozingatia vyakula
mchanganyiko na ushiriki mdogo wa akinababa katika ufuatiliaji wa makuzi na
maendeleo ya mtoto hivyo kumwachia mama majukumu yote. Na wakina mama
wajawazito kuanza kliniki ya uzazi kwa kuchelewa.
Alisema kuwa changamoto hizo ziliifanya Ofisi ya Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na wadau
kuandaa shindano la Mama Msosi Lishe litakalohusisha wanawake watakao andaa
chakula bora cha familia. Aliongeza kuwa katika uandaaji huo, watapimwa uelewa
wao juu ya umuhimu wa lishe bora, usafi wa mazingira yanayomzunguka na matumizi
ya nishati mbadala ili kupunguza uharibifu wa mazingira.
Kampeni ya Mama Msosi Lishe
mwaka 2017 inaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘Mama Msosi lishe’. Chimbuko lake ni
kupambana na utapiamlo hasa udumavu kutokana
na Mkoa wa Iringa kuwa miongoni mwa
Mikoa 5 ya Tanzania yenye kiwango kikubwa cha udumavu, kwa mujibu wa utafiti wa
viashiria vya afya (TDHS, 2015/2016) ukiwa na asilimia 42 ya udumavu.
=30=
No comments:
Post a Comment