Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Timu
ya mpira wa miguu ya RAS Iringa imechapwa magoli 5-0 na wakala wa Barabara (TANROADS) katika mechi ya
ufunguzi iliyoshuhudiwa na mamia wa wakazi wa Manispaa ya Iringa wakiongozwa na
Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela.
Mechi
hiyo iliyochezwa katika dimba la chuo cha Ualimu Kleruu kilichopo manispaa ya
Iringa ilianza kwa kasi ndogo huku kila timu ikosoma mchezo wa mwezake. Hadi
kipinci cha kwanza kinaisha timu ya RAS IRINGA ilikuwa nyuma kwa goli Moja. Kipindi
cha pili kilianza kwa kasi kidogo.
Jitihada za RAS IRINGA kurudisha goli
zilionekana wazi kabla ya juhudi hizo kufifishwa baada ya golikipa wao namba moja
Mashaka Mwanage kuumia mkono wa kuume na kushindwa kuendelea na mchezo. Pigo
hilo kwa RAS IRINGA lilifungulia mvua ya magoli hadi kufikia magoli matano.
Tangu
awali TANROADS walionekana kukamia mechi hiyo huku wakiwa na kikundi cha
washangiliaji mahili. Muda wote wa mchezo meneja wa TANROADS Mhandisi Daniel
Kindole alikuwa akifuatilia kwa makini mechi hiyo.
Baada
ya kipeng cha mwisho watumishi wa RAS walionekana kuondoka mmoja mmoja kwa njia
yake jambo lililotafsiriwa na wachambuzi wa masuala ya soka kuwa ni kuvurugwa
na kichapo hicho.
=30=
No comments:
Post a Comment