Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Watumishi
wa taasisi mbalimbali mkoani Iringa wametakiwa kucheza kwa nidhamu na kuepuka
ugomvi katika mashindano ya mpira wa miguu yanayoendelea mkoani Iringa.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika hotuba yake ya
ufunguzi wa mchezo wa mpira wa miguu kwa taasisi za mkoa wa Iringa iliyosomwa
kwa niaba yake na mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela katika uwanja wa
chuo cha ualimu Kleruu kilichopo Manispaa ya Iringa jana.
Masenza
aliwataka wachezaji hao kucheza kwa nidhamu na kuepuka kuchochea ugovi. Alisema
kuwa mchezo wa mpira wa miguu ni burudani na unajenga urafiki hivyo, mashindano
hayo yatumike kutoa burudani na kujenga urafiki miongoni mwa wanamichezo hao.
Aliongeza
kuwa mashindano hayo yatumike kujenga uzalendo kwa watumishi wa umma na
watumishi wa taasisi zisizo za kiserikali mkoani Iringa. Aidha, aliwataka
wanamichezo hao kutengeneza mtandao utakaowaunganisha kama wanamichezo na
watumishi wa taasisi mbalimbali.
Katika
salamu za afisa michezo Mkoa wa Iringa, Kenneth Komba kabla ya kumkaribisha
mgeni rasmi, alisema kuwa michezo hiyo ni wazo la mkuu wa Mkoa wa Iringa kutaka
kuwaunganisha watumishi wa taasisi za Mkoa wa Iringa kupitia mchezo wa mpira wa
miguu. Alisema kuwa hadi kufikia jana jumla ya taasisi 21 zilikuwa zimejitokeza
kushiriki mashindano hayo.
Wakati
huohuo, mechi ya ufunguzi, timu ya Timu ya RAS Iringa ilikubali kichapo cha
magoli 5 bila kutoka TANROADS.
Mashindano
ya mpira wa miguu kwa taasisi za Mkoa wa Iringa ni mashindanao ya kwanza ya
aina yake kufanyika mkoani hapa yakikabiliwa na changamoto ya udhanimi.
=30=
No comments:
Post a Comment