Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
Maafisa ugani katika maeneo yanayolima zao la korosho wilayani
Iringa wametakiwa kutimiza wajibu wao katika kukifanya kilimo cha korosho kuwa
chenye tija.
Kauli hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza
alipokuwa akizindua kilimo cha zao la koroso katika kijiji cha Idodi wilayani
Iringa jana.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa aliwataka maafisa ugani na viongozi
wa serikali kuanzia ngazi ya kijiji hadi tarafa wa maeneo yanayolima zao la
korosho kutimiza wajibu wao katika kulifanya zao hilo kuwa na tija.
“Tunataka Mkoa ufanikiwe katika kilimo cha
zao hili na ushauri wangu itungwe sheria ndogo itakayomlazimisha kila mkulima
kushiriki katika kilimo hiki kinachotarajiwa pia kuchochea uanzishwaji wa
viwanda vya kubangua korosho,” alisema mkuu wa Mkoa.
Vilevile,
aliwataka viongozi hao kuanzisha mashamba darasa yatakayotumika kihamasisha
wananchi na kutumika kwa mafunzo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa,
Robert Masunya alisema kuwa Halmashauri yake imezalisha miche 69,855
itakayotolewa bure kwa shule za msingi na sekondari na wananchi walio tayari
kwa mashamba yao kupandwa. Alisema kuwa bodi ya korosho imedhamini upatikanaji
wa miche hizo ili kuhamasisha zao hilo wilayani Iringa.
Masunya alisema kuwa katika awamu ya kwanza ya
utekelezaji wa mpango huo shule za msingi zitapewa miche 3,672 itakayopandwa
katika mashamba ya ekari 136. Aliongeza kuwa eneo la ekari 14 linalomilikiwa
shule za sekondari litapandwa miche 378. Aliongeza kuwa wananchi watapewa miche
65,803 itakayopandwa katika eneo la ekari 2,437.
Vijiji
vitakavyo zao la korosho linaweza kustawi ni Idodi, Mahuninga, Mlowa,
Ilolompya, Mlenge, Itunundu, Kising’a, Kihorogota, Nyang’oro, Nzihi na Kiwele.
=30=
No comments:
Post a Comment