Thursday, July 25, 2013
Wednesday, July 24, 2013
TAFRIJA YA KUMPONGEZA LCPL ELIAS ADRIANO MBEGA KWA KUPANDISHWA CHEO
CPL William Kibasa (kushoto) na CPL Richard Mtove (kulia) wakifuatilia matukio ya hafla hiyo.
SGT Felister Maginga (kulia) na PTE Dorah Kibiki (kushoto) wakifuatia matukio ya hafla hiyo.
LCPL Elias Adriano Mbega akiwashukuru Maafisa, Snrnco Maaskari kwa kumuandalia tafrija ya kupandishwa cheo.
COL. SV. Shayo Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Iringa akiteta jambo na CPL Goodluck Mwasubila.
LCPL Elias Adriano Mbega akifurahia hafla yake ya kupandishwa cheo.
CGT Felister Maginga akisalimia
CPL. Goodluck Mwasubila akibadilishana mawazo na Afisa Ugavi wa Mkoa Janeth Kitinye.
LCPL Elias Adriano Mbega akibadilishana mawazo na mate wake PTE. Dorah Kibiki.
Tuesday, July 23, 2013
SALAMU ZA RC IRINGA KATIKA MAZISHI YA MWANAJESHI ALIYEFARIKI DARFUR -SUDAN
Salamu za Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma (Mb.) katika mazishi ya CPL Osward Paulo Chaula amesema yafuatayo:
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine G. Ishengoma (Mb.) akitoa salamu za Mkoa wa Iringa
Wanajeshi wakitoa heshima zao kwa marehemu CPL. Osward Paulo Chaula
Kwa
masikitiko makubwa kwa niaba ya wananchi wa mkoa wa Iringa, napenda
kutoa poke kwa familia ya Paulo Chaula kwa kufiwa na kijana wetu askari
CPL.Osward Paulo Chaula, ambaye alikuwa akishiriki ulinzi wa amani
nchini Darfur, Sudan.
Tukio hilo lilitokea tarehe 13 Julai, 2013.
Mkoa
wa Iringa na Taifa kwa ujumla, tunakiri kwamba tumeondokewa na kijana
wetu shujaa, mzalendona mchapa kazi ambaye umauti umemkumba akiwa
kazini. askari huyu alikuwa tegemeo kubwa kwa Taifa letu la Tanznaia.
Tunaahidi tutayaenzi yale yote mazuri aliyotuachia watanzania.
kutokana
na tukio hilo, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa pamoja na Ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Kilolo zinatoa pole ya Tshs. 500,000/= kwa familia ya Paulo
Chaula.
=30=
MATUKIO KATIKA PICHA YA MAZISHI YA MWANAJESHI ALIYEFARIKI DARFUR NCHINI SUDAN
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt Christine G. Ishengoma (Mb.) akisaini kitabu cha wageni katika mazishi ya CPL.Osward Paulo Chaula
Baadhi ya waombolezaji wakipita kutoa heshima zao za mwisho mbele ya mwili wa marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Waombolezaji wakiomboleza kifo cha CPL.Osward Paulo Chaula
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiaga mwili wa marehemu
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Mhe. Gerald Guninita akiaga mwili wa marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa akiaga mwili wa marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakiaga mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wenzake wa Jeshi la Wananchi wakibeba jeneza lenye mwili wamarehemu wa CPL.Osward Paulo Chaula
Wanajeshi vijana wa JWTZ wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula
Mwili wa CPL.Osward Paulo Chaula ukipelekwa makaburini
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiweka udongo katika kaburi alimolala marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Bibi Scolastica Mlawi akiweka udongo katika kaburi alimolala marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Waombolezaji wakiomboleza kifo cha CPL.Osward Paulo Chaula
Wapiganaji wa JWTZ wakiendelea na taratibu za kijeshi katika mazishi
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akiweka Shada la ua katika kaburi alimolala marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (Mb.) akikabidhi rambirambi kwa familia ya marehemu CPL.Osward Paulo Chaula
Sunday, July 21, 2013
MDAHALO WA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA WASOMI
TANGAZO LA MDAHALO
Mkurugenzi
Mtendaji wa Asasi isiyo ya kiserikali ya Community
Integrated Communication and Culture (CICC) anawatangazia vijana wote
wahitimu wa vyuo vikuu na wanaosoma katika vyuo vikuu nchini kujitokeza
kushiriki katika mdahalo wa fursa za Ajira nchini.
MADA
itakayojadiliwa ni Mchango wa Vijana
wasomi katika upatikanaji wa Ajira nchini.
Mdahalo
huo utafanyika katika ukumbi wa Highland,
Iringa siku ya Jumanne tarehe 23/07/2013
kuanzia saa 4:00Asubuhi hadi saa 6:00 Mchana.
Vijana
wote waliohitimu vyuo vikuu na wanaosoma katika vyuo vikuu nchini
mnakaribishwa.
Mzungumzaji
Mkuu katika Mdahalo huo atakuwa Mhe.
Mch. Peter Msigwa- Mbunge wa Iringa Mjini.
HAKUNA KIINGILIO
Kwa
mawasiliano zaidi wasiliana na;
Bi.
Neema Mwamoto,
Mkurugenzi
Mtendaji CICC
SLP
554, Iringa
Mob:
0752090900,
Friday, July 19, 2013
RC ATAKA JAMII ISHIRIKISHWE KATIKA UTUNZAJI WA BARABARA
Serikali mkoani Iringa imetaka jamii ishirikishwe ipasavyo
juu ya dhana ya utunzani wa barabara ili kuhakikisha barabara zinadumu na
kupitika muda wote.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt.
Christine Ishengoma wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa
Iringa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo mjini Iringa.
Dkt. Christine amesema “katika kuhakikisha tunakuwa na
barabara zinazopitika muda wote, nimeona mapungufu ya ushiriki wa jamii juu ya
utunzaji wa barabara hizo. Wananchi wamekuwa wakifanya shughuli ndani ya
hifadhi ya barabara na kuacha uchafu kwenye barabara na uchafu huo kuziba
mifereji na kuharibu barabara”. Aidha, amewataka wajumbe wa kikao hicho kutoa
elimu kwa wananchi ili washiriki kikamilifu katika utunzaji wa barabara hizo
ili ziweze kudumu na kuwahudumia kwa muda mrefu. Amesema kuwa uchafu unaharibu
mazingira, unaziba mifereji ya barabara na kusababisha mafuriko kwenye makazi
ya wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Iringa ametoa rai kwa viongozi na wananchi
kushirikiana na miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara ya Iringa –Dodoma na
Iringa-Mafinga. Amesema kuwa ushirikiano huo na elimu kwa wananchi utasaidia
kukomesha hujuma za wizi hasa wa mafuta na ementi ili miradi hiyo iweze kuwa ya
manufaa kwa mkoa wa Iringa na taifa kwa ujumla na kukamilika kwa muda muafaka.
Aidha, amewataka wajumbe hao kuendela kushirikiana katika
kutoa elimu kwa wananchi juu ya Sheria mpya ya hifadhi ya barabara ambayo ni
mita 30 kil upande kutoka katikati ya barabara. Amesema “wananchi waendelee
kuelimishwa juu ya umuhimu wake kwani wanapojenga na kubomolewa nyumba zao
haipendezi. Inawagharimu na kuwaumiza sana” alisisitiza Mkuu wa mkoa wa Iringa.
=30=
Subscribe to:
Posts (Atom)