Wednesday, September 22, 2010

Amani na Utulivu kazi ya matokeo ya CCM
Mgombea urais akumbusha amani na utulivu watanzania wanaojivunia leo hii ni matokeo ya sera nzuri za chama cha mapinduzi zisizolenga ubaguzi wa aina yoyote kwa raia wake imeelezwa.
Kauli hiyo imeelezwa na mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa tiketi ya chama cha mapinduzi (CCM) Jakaya Kikwete katika uwanja wa Samora mjini Iringa.
Kikwete amesema “sema nzuri za chama cha mapinduzi zisizobagua raia wake hali zao, rangi, dini, kabila, ndiyo misingi ya amani tuliyonayo”. Ameongeza kuwa CCM ni waaminifu na wakiahidi wanatekeleza na yote ya msingi waliyoahidi wameyatekeleza isipokuwa kidogo sana.


Mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete akiwa na Fredrick Mwakalebela katika uwanja wa Samora
Akizungumzia changamoto za elimu, mgombea urais wa CCM amesema serikali imejipanga kukabiliana na upungufu wa waalimu, maabara, vitabu na nyumba za walimu. Amesema kuwa serikali ya awamu ya nne imeamua kujenga chuo kikuu cha Dodoma na kitakapokamilika kitadahili wanafunzi 40,000 na kati yao 15,000 ni waalimu. Mkakati mwingine wa kuongeza waalimu ameutaja kuwa ni kuviomba vyuo binafsi kuongeza udahili wa wanafunzi wa fani ya ualimu nchini na pindi wanapohitimu serikali itawaajiri. Kikwete amesema kuwa kila shule ya sekondari itapata walimu wasiopungua watano. Mkakati mwingine katika elimu ameutaja kuwa ni kujenga uwezo wa ndani ili kuchapisha vitabu ndani ya nchi. Akizungumzia wafadhili wan je katika elimu amesema kuwa tayari Tanzania imepata vitabu 800,000 toka nchini Marekani na vingine 2,400,000 vipo njiani kufikia mwezi Februari, 2011.
Mgombea huyo urais kupitia tiketi ya CCM amesema lengo la serikali yake ni kuhakikisha kila mwanafunzi anakuwa na kitabu chake cha hisabati, phisikia, chemia na biolojia ifikapo mwaka 2011/ 2012.
Naye mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya chama cha mapinduzi, Monica Ngenzi Mbega akielezea mafanikio ya serikali ya awamu ya nne katika utekelezaji wa Ilani ya CCM amesema kuwa wakazi wa Manispaa ya Iringa wananufaika na mtandao wa maji kwa asilimia 95 mwaka 2010 ukilinganisha na asilimia 72 mwaka 2005.
Kwa upande wa elimu Mbega amesema kuwa shule za sekondari zimeongezwa kutoka shule 5 (2005) hadi shule 13 (2010) sambamba na wanafunzi wanaomaliza kutoka 930(2005) hadi 14,970 (2010).
Uwanja wa Samora ulirindima kwa shangwe pale alipopanda jukwaani aliyekuwa mshindi katika kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi na kuenguliwa Fredrick Mwakalebela alipopanda jukwaani na kutangaza rasmi kuvunja kundi lake na kutangaza kumuunga mkono mgombea ubunge wa jimbo la Iringa Mjini, Monica Mbega “kwa sasa naelekeza nguvu zote kwa Monica Mbega kama mgombea ubunge, madiwani wote na mgombea urais wa CCM”. Mwakalebela alichukua nafasi hiyo kuwaasa wanasiasa waotumia jina lake jukwaani kumsikitikia na kusema waache mara moja na wasimtumie kama sera yao.
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano kupitia chama cha mapinduzi yupo mkoani Iringa katika ziara ya siku nne ya kampeni za urais, ubunge na udiwani.  

Thursday, September 9, 2010

Maziwa ya mama hujenga mahusiano kati ya mama na mwana

Maziwa ya mama ndiyo chakula pekee na cha asili kinachompa mtoto afya na nguvu na kinasaidia kujenga uhusiano mwema baina ya mamam na mtoto imeelezwa.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Muuguzi wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa, Aida Kapwani wakati akiwafundisha akina mama waliohudhuria kliniki ya watoto wachanga mada ya afya ya mama na mtoto katika hospitali ya mkoa wa Iringa leo.

Kapwani amesema “kitendo cha mama kunyonyesha mtoto wake maziwa ya mama kinamfanya mtoto awe na afya njema na nguvu sababu maziwa ya mama ni chakula kamili na cha asili kwa mtoto mchanga”. Ameongeza kuwa unyonyeshaji wa maziwa ya mama unamjenga mtoto kisaikolojia na kuuisha uhusiano baina ya mama na mtoto.

Kapwani amesisitiza kuwa pasina sababu yoyote au maelekezo yoyote toka kwa daktari ni lazima mtoto anyonye maziwa ya mama pekee kwa kipindi chote cha miezi sita mfululizo bila kuchanganya na kitu chochote. Amesema “maziwa ya mama ni chakula kamili na kinywaji cha kwanza kwa mtoto mchanga”.

Akielezea faida za maziwa ya mama kwa mtoto mchanga, Kapwani amesema kuwa yanamuondolea mtoto hatari ya kushambuliwa na magonjwa kama vile utapiamlo, kuhara, kutapika na kudumaa. Faida nyingine ameitaja kuwa ni mtoto kupata virutubisho vyote stahili vya mwilini. Aidha ameongeza kuwa faida nyingine ya mama kunyonyesha mtoto maziwa ya mama kunamuwezesha mama kutopata upungufu wa damu na maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Katika darasa la kliniki hiyo lililohudhuriwa na akina mama zaidi ya hamsini, Kapwani alikatishwa taa na ushiriki na muitikio wa akina baba katika elimu ya afya ya mama na mtoto ikiwa ni pamoja na kuhudhuria kliniki. Aidha alichukua fursa hiyo kuwapongeza akina baba wawili aliohudhuria darasa la klini hiyo na kutoa wito kwa akina baba wote kuwasindikiza wake zao pindi wanapoenda klinini na kupatiwa mafunzo ya afya ya uzazi wa mama na mtoto.

Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa ambayo akina baba wanamuitikio hafifu sana wa kuhudhuria kliniki ya afya ya uzazi wa mama na mtoto.


Picha ya mtoto akitumia haki yake hotelini

Tuesday, September 7, 2010

‘IRINGA YATAKIWA KUWA KINARA KATI YA MIKOA 6’

Mkoa wa Iringa umetakiwa kuwa kinara kwa mafanikio kati ya mikoa sita inayotekeleza mradi wa kuimarisha minyororo ya thamani kwa mazao (MUVI).


Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka katika hotuba yake ya ufunguzi wa warsha ya kuandaa mpango wa uwekezaji katika mradi wa kuimarisha minyororo ya thamani kwa mazao ya Alizeti na Nyanya iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha ufundi stadi (VETA).


Mpaka amesema “Iringa lazima tuwe wa kwanza kwa mafanikio kati ya mikoa sita inayotekeleza mradi wa MUVI”. Ameitaja mikoa inayotekeleza mradi wa MUVI kuwa ni Ruvuma, Pwani, Tanga, Manyara, Mwanza na Iringa yenyewe. Ameongeza kuwa ili kufanikiwa lengo hilo la kuwa wa kwanza kimafanikio lazima wadau wote wanaohusika na utekelezaji wa mradi huo kufanya kazi kama timu moja.


Katibu Tawala huyo wa Mkoa amesema kuwa upande wa serikali ya mkoa itahakikisha inatoa mchango na usimamizi wote unaohitajika kama ilivyo kawaida ya mkoa kuwa karibu na kushirikiana na wadau wake wa maendeleo. Aidha amewataka wakurugenzi na wadau wote kuhakikisha kuwa mradi wa MUVI unaoanishwa na mipango ya wilaya kama DADPs kadri itakavyowezekana kuanzia mwaka wa fedha 2011/2012.


Aidha amewataka wakulima kutambua kuwa wao ndio walengwa wakuu wa mradi hivyo wazaleshe kibiashara ili waweze kujikomboa kiuchumi. Amesisitiza kuwa mradi hauji kugawa fedha bali ni kuwajengea uwezo kiutaalamu na kuwaunganisha pamoja ili kuangalia maslahi yao kwa upana zaidi.


Ametumia warsha hiyo kuwaomba washiriki wote kushiriki kikamilifu na kuibua masuala yote ya msingi na kuyatengenezea mkakati, rasilimali na muda wa utekelezaji.


Kwa mujibu wa taarifa za maendeleo ya kilimo ya mkoa na FAO mkoa wa Iringa unazalisha zaidi ya asilimia 70% ya nyanya zinazozalishwa nchini Tanzania. Mkoa pia unaviwanda viwili vikubwa vya kusindika nyanya vyenye uwezo wa kusindika tani 15 kwa siku. Mkoa wa Iringa unazalisha zaidi ya tani 18,000 za mbegu za alizeti kwa mwaka.


Warsha hiyo imeandaliwa na SIDO na MUVI na imewaleta pamoja wadau muhimu ili kuamua kwa pamoja ufanisi wa minyororo ya mazao ya alizeti na nyanya mkoani Iringa.






FAMILIES MOURN AS DEATH TOLL CLIMBS IN GUATEMALALANDCLIDES

By the CNN Wire Staff
September 7, 2010 7:40 a.m.



Relatives of missing people wait Sunday in Solola, west of Guatemala City, near the site of a recent landslide.


STORY HIGHLIGHTS


• One family mourns four dead


• The president declares three days of national mourning


• Emergency officials report 44 dead, 56 injured and 16 missing


• About 11,500 people have been evacuated and 9,000 are living in shelters


Nahuala, Guatemala (CNN) -- Officials say about 40 people were buried in two landslides here. Four of them were Carlos Coti's family members.


"They left behind 20 orphans, because each one had four, five or six children they left behind," he said.


The first landslide knocked a number of vehicles and a bus off the road. When nearby residents rushed to the scene to help, a second mudslide crashed down on the same spot, the nation's disaster agency said.


Constant rains have forced rescue crews to stop and restart their searches for the missing, as anxious family members look on.


Disaster officials report that torrential rains and landslides have left at least 44 dead, 56 injured and 16 missing. On Monday, President Alvaro Colom declared three days of national mourning.




Video: Mudslides cause havoc in Guatemala


"The firefighters and rescue teams are working with the government's equipment so that we can come out of this human tragedy," Colom said as he visited one landslide site.


Around 11,500 residents have been evacuated and 9,000 have taken refuge in shelters, the nation's disaster agency said. More than 43,000 people are at risk from the punishing rain, said to be the strongest in 60 years.


Over the weekend, authorities closed parts of the Inter-American Highway after rains washed out sections of the road and caused at least two accidents.


Thousands of homes, in addition to infrastructure and fields of crops, also were damaged by the heavy rains.


The torrential downpours come several months after more than 150 people died when Tropical Storm Agatha hit Guatemala in May.


Destruction from that storm was widespread throughout the nation, with mudslides destroying homes and buildings and burying some victims. At least nine rivers had dramatically higher levels and 13 bridges collapsed, Guatemala's emergency services agency said.


The May downpours created a sinkhole the size of a street intersection in northern Guatemala City. Residents told CNN that a three-story building and a house fell into the hole.


Journalist Alexia Rios Hayashi contributed to this report.

Sunday, September 5, 2010

China's monster traffic jam rears its head again

China's monster traffic jam rears its head again



AP – In this photo taken on Monday, 2010, a truck driver washes himself after waiting over four days …



BEIJING – China's monster traffic jam has reared its head again, with trucks and cars backed up for up to 18 miles (30 kilometers) Saturday on a highway north of Beijing, although that is a third the size of what it was.

The traffic jam came four days after the break-up of an even bigger one — stretching to 60 miles (100 kilometers) at one point.

State media said the latest jam on the Beijing-Tibet highway was caused by an accident and road maintenance.

The worst of the jam started in Zhangjiakou, a city about 90 miles (150 kilometers) northwest of Beijing, and stretched into Inner Mongolia in northern China, with traffic creeping along in fits and starts.

A woman who answered the phone at the Beijing traffic management office said drivers should not take the highway. "The traffic flow is very slow," said the woman, who refused to give her name.

Traffic jams are part of daily life in China's major cities, with vehicles moving at a crawl in parts of Beijing for most of the day.

In the last traffic jam on the Beijing-Tibet highway, which started Aug. 14 and lasted about 10 days, state media said some drivers were stuck for five days with drivers on the worst-hit stretches passing the time sitting in the shade of their immobilized trucks, playing cards, sleeping on the asphalt or bargaining with price-gouging food vendors.

A bottle of water was selling for 10 yuan ($1.50), 10 times the normal price, Chinese media reports said.

The main reason traffic has increased on the partially four-lane highway is the opening of coal mines in the northwest, vital for the booming economy, which this month surpassed Japan's in size and is now second only to America's.

Officials eased the first jam by directing truckers to take a 180-mile-long (300-kilometer-long) detour, the China Daily said.

It quoted one truck driver, Lu Yong, who was stuck in both jams, as saying he should have prepared some food this time. "Who knows when the traffic will move again?" said the 37-year-old, who was stranded for two nights in the last jam at almost the same location.

A woman at the Inner Mongolian traffic management office said it may take several days to ease the latest jam. "Please do not drive on this expressway," said the official, who also would not give her name.

From AP

Saturday, September 4, 2010

wanafunzi 45,104 kufanya mtihani wa darasa la Saba Iringa

Jumla ya wanafunzi 45,104 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka huu 2010 mkoa ni Iringa imeelezwa.


Mwl. Leonard Msigwa, Afisa Elimu Takwimu Mkoa wa Iringa


Takwimu hizo zimetolewa na Afisa Elimu –Taaluma wa mkoa wa Iringa, Ndg. Leonard Msigwa katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii ofisini kwake leo.


Ndg. Msigwa amesema “wanafunzi wanaotarajia kumaliza elimu ya msingi katika mkoa wa Iringa jumla yao ni 45,104”. Ameongeza kuwa kati yao wasichana ni 23,620 na wavulana ni 21,484.


Afisa Elimu taaluma amesema kuwa mkoa unao wanafunzi wasioona 13 wanaotumia maandishi ya vinundu na kati yao 8 ni wavulana na 5 ni wasichana. Amezitaja shule wanazosoma kuwa ni shule ya msingi Mwaya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo (wanafunzi 3) na Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi (wanafunzi 10). Aidha ameongeza kuwa mkoa unao wanafunzi wenye uoni hafifu 20 katika shule 8 tofauti na kati yao wasichana ni 10 na wavulana ni 10. ameongeza kuwa Halmashauri ya Manispaa ina shule 3 zenye wanafunzi (13), Halmashauri ya Wilaya ya Makete wanashule 2 zenye wanafunzi (4), Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi wanashule 2 zenye wananfunzi (2) na Njombe Mji wanashule 1 yenye mwanafunzi (1).


Kwa upande wa maandalizi amesema kuwa maandalizi yote yamekamilika na kusema “mitihani yote imekamilika kadri ya mahitaji na kuna ziada ya bahasha zaidi ya 70 kwa kila somo”. Aidha zoezi la kusambaza mitihani hiyo kwa kila Halmashauri limekamilika jana jioni.


Ndg. Msigwa ameongeza kuwa elimu imetolewa kwa maafisa elimu wa wilaya zote za mkoa wa Iringa na kuapishwa kwa Maafisa Elimu msingi, Maafisa Elimu sekondari na wataaluma wote wa msingi na sekondari juu ya kutunza mitihani, pia wasimamizi watakao kuwa madarasani wote wataapishwa.


Kuhusu wizi na uvujaji wa mihihani amesema kuwa umefanyika mchakato makini wa kuwapata watu waadilifu kwa kushirikiana na usalama wa taifa na makamanda wa polisi wa wilaya zote. “Wasimamizi wazembe wote wamezuiliwa kusimamia sababu kumbukumbu zao zipo wazi” amesisitiza.


Mkoa wa Iringa una jumla ya shule za msingi 850 na mtihani wa kumaliza elimu ya msingi (PSLE) mwaka 2010 utaanza tarehe 6 Septemba, 2010 kwa masomo ya Sayansi, Hisabati na Kiswahili na kuendelea siku ta tarehe 7 Septemba, 2010 kwa masomo ya Kiingeleza na Maarifa ya Jamii.

Friday, September 3, 2010

Mama Mpaka asisitiza elimu kwa wapiga kura pasina itikadi za kisiasa

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa amekitaka chuo kikuu cha Tumaini Iringa kutoa elimu ya manufaa kwa wapiga kura pasipo kuingiza itikadi zinazolenga upande fulani wa chama chochote cha siasa.


Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Mama Gertrude Mpaka

Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha ya siku moja ya elimu ya mpiga kura kwa wilaya ya Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa chuo cha ushirika tawi la Iringa.

Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, mama Gertrude Mpaka amesema “nawakata mtoe elimu ya manufaa kwa wapiga kura bila kuingiza itikadi zinazoelekea upande fulani wa chana chochote”. Ameongeza kwa kuwataka wafundishe mambo yote kwa mujibu wa mada zilizopitishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na si vinginevyo.

Mama Mpaka amesisitiza kuwa elimu kwa wapiga kura ni muhimu sana kwa wananchi wote hasa waishio vijijini kwa sababu wananchi wengu wa vijijini hudanganywa wasichiriki katika uchaguzi. Aidha ameongeza kuwa elimu hiyo itawasaidia wananchi wengi kutokushawishiwa kuuza shahada zao za kupigia kura wala kushawishiwa kushiriki kuleta fujo wakati wa kampeni au uchaguzi na kufanya hivyo ni kinyume na sheria.

Katibu Tawala huyo wa mkoa wa Iringa amewataka wananchi wa Mkoa wa Iringa kutunza kadi zao za kupiga kura kama mboni ya jicho. Amesema “kadi hii inakupa utu, inakupa haki ya kumchagua kiongozi, unayemtaka na unayeona anafaa kuwa kiongozi”. Aidha amechukua nafasi hiyo kuwataka wananchi wa Iringa ifikapo tarehe 31 Oktoba, 2010 kwenda kupiga kura.

Amewataka waandaaji wa warsha hiyo kuwaeleza wananchi kuwa kila raia anayo haki ya kuchagua, kuchaguliwa na kusikilizwa anapotoa maoni yake kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika kampeni kusikiliza sera za wagombea ili kuwa na uelewa mpana wa sera na ilani za wagombea wate wa nafasi za uongozi.

Mama Mpaka amewakumbusha watumishi wa umma kuzingatia Waraka waMkuu wa Utumishi wa Umma Na. 1 wa mwaka 2000 unaohusu maadili ya watumishi wa umma katika mfumo wa vyama vingi vya siasa kuwa unawataka watumishi wa umma kutojihusisha na siasa mahali pa kazi.

Amewataka washiriki wa warsha hiyo kuzingatia mafundisho watakayoyapa na kwenda kuwafundisha wengine kwa usahihi mkubwa bila upotoshaji wa makusudi. Amekumbusha kuwa serikali imekemea vitendo vyovyote vya rushwa wakati wa uchaguzi na kuwataka wawe wasimamiaji wa sera na sheria za taifa zenye kudhibiti vitendo hivyo.

Warsha hiyo imeandaliwa na chuo kikuu cha Tumaini- Iringa baada ya kushinda tenda ya shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) inayosimamiwa na shirika la DELOITTE. Warsha hiyo inawahusisha maafisa watendaji wa kata za Kalenga, Nzihi, Ulanda, Mseke, Nduli, Nyang’oro na Kihorogota. Wengine ni walimu wa masomo ya uraia na waandishi wa habari kwa uwiano wa kijinsia.


Washiriki wa warsha ya elimu ya mpiga kura wilaya ya Iringa akisikiliza kwa umakini hotuba ya mgeni rasmi mama Gertrude Mpaka katika ukumbi wa chuo cha ushirika Iringa.

Wednesday, September 1, 2010

RAS Iringa awaweka sawa watumishi wake

Wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa wametakiwa kuchukua tahadhari na jitihada za dhidi ya majanga ya moto yanayoweza kujitokeza katika ofisi hiyo.
Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Gertrude Mpaka akiongea na wafanyakazi wake


Tahadhali hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Mkoa huo, Gertrude Mpaka katika kikao baina yake na wafanyakazi wote wa ofisi yake kilichofanyika leo katika ukumbi wa RAS.

Mpaka amesema “nimewaita hapa ili tuelezane na kuchukua hatua za tahadhari katika ofisi zetu na matumizi sahihi ya vifaa vinavyotumia umeme ili moto usitokee na kuunguza ofisi”. Ameongeza kuwa kila mfanyakazi lazima ahakikishe anazima vifaa vyote vya umeme pindi amalizapo kazi na kutenganisha kebo za umeme na soketi za ukutani. Aidha amesisitiza kuwa kikao hicho anakipa umuhimu mkubwa japokuwa ofisi yake imekuwa ikiwakumbusha mara kwa mara wafanyakazi wake kuchukua tahadhari na matumizi sahihi vya vifaa vya moto.

Akiongelea hali ya usalama katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mwangalizi wa Ofisi, Avelyne Ngonyani, amesema kuwa hali ya usalama katika ofisi hiyo ni ya kuridhika baada ya kujiwekea mikakati kadha wa kadha ya kuimarisha usalama. Ngonyani amechukua nafasi hiyo kuwakumbusha wafanyakazi wote kuwa lazima funguo zote za ofisi zihifadhiwe katika ‘combination locks’. Ameongeza kuwa katika kuimarisha usalama kila mfanyakazi lazima asaini kitabu cha mahudhuria pindi aingiapo ofisini na baada ya muda wa kazi pia.

Akichangia katika usalama wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu, Barnabas Ndunguru amesisitiza kuwa funguo za ofisi ni nyaraka za serikali na ni kosa kwa mfanyakazi yeyote kuondoka na funguo hizo. Aidha amesisitiza kuwa endapo mfanyakazi atahitaji kufanya hivyo au kuendelea na kazi baada ya muda wa kazi basi hanabudi kuomba kibali kutoka kwa mkuu wa utawala ofisini hapo.

Katibu Tawala Mkoa pia amegusia kuwa nchi ipo katika kampeni za uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2010 na kusisitiza kuwa “joto la kampeni za uchaguzi limeanza, hivyo wafanyakazi hatutakiwa kushabikia siaka katika ofisi za umma na katika muda wa kazi japokuwa tuna vyama vya siasa”. Mpaka amechukua nafasi hiyo kuwatakia maandalizi mema ya uchaguzi mkuu na kuwataka wafanyakazi wote wajitokeze kupiga kura.


Baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya RAS Iringa wakimsikiliza RAS wao leo