...Ongezeko la asilimia 102 Mapato ya Serikali
Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali za Mitaa umeongezeka hadi kufikia 102% katika kipindi cha Mwaka 2009/2010 kutokana na Mapato ya ndani ya Halmashauri za Wilaya katika Mkoa wa Iringa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Utekelezaji Mpango wa Maendeleo na Bajeti kwa Mwaka 2009/2010 na Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo na Bajeti Mwaka 2010/2011 iliyowasilishwa na Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Mipango na Uratbu, Nuhu Mwasumile katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) kulichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Mwenyekiti wa RCC Mhe. Issa Machibya (kulia) na Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Anne Makinda
Mwasumilwe amesema kuwa Serikali za Mitaa katika kipindi cha Mwaka 2009/2010 zilikadiliwa kukusanywa kiasi cha Shs. 4,613,991,146 kutokana na vyanzo vyake vya ndani (own source). Amesema kuwa hadi kufikia Mwezi Juni, 2010, jumla ya Shs. 4,674,992,320.43 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 102. Kwa Mwaka 2010/2011 Serikali za Mitaa ziliidhinishiwa kiasi cha Shs. 98,623,349,000. Kati ya fedha hizo Shs. 70,809,941,000 ni kwa ajili ya Mishahara na Shs. 27,813,408,000 kwa ajili ya matumizi mengine.
Aidha, katika kipindi cha Mwaka 2009/10, Sekretarieti ya Mkoa ilikadilia kukusanya jumla ya Shs. 1,146,000 ikiwa ni Mapato ya Serikali kuu. Hadi kufikia Mwezi Juni, 2010, jumla ya Shs. 260,565,459.70 zimekusanywa.
Mwasumilwe amesema kuwa kwa Mwaka wa fedha 2009/2010, Mkoa uliidhinishiwa jumla ya Shs. 117,061,090,126 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Katika fedha hizo Shs. 87,742,207,575 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shs. 29,318,882,551 kwa ajili ya kugharamia Miradi ya Maendeleo. Katika kipindi hicho Sekretarieti ya Mkoa iliidhinishiwa jumla ya Shs. 6,400,957,000 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo Shs. 3,362,957,000 ni kwa ajili ya Mishahara na Shs. 3,038,000,000 kwa ajili ya Matumizi mengineyo. Aidha, kwa Mwaka 2010/2011 Sekretarieti ya Mkoa iliidhinishiwa jumla ya Shs. 6,633,520,000 kwa ajili a Matumizi ya kawaida. Kati ya hizo Shs. 4,010,228,000 ni Mishahara na Shs. 2,623,292,000 ni Matumizi mengine.
Vilevile kwa Mwaka 2010/2011 Mkoa wa Iringa uliidhimishiwa kutumia jumla ya Shs. 142,573,623,000 kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Maendeleo. Kati ya hizo Shs. 256,869,000 ni kwa ajili ya Matumizi ya kawaida na Shs. 37,316,754,000 kwa ajili ya kugharamia Miradi ya Maendeleo.
Katika ufunguzi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kanali Issa Machibya amezungumzia hali ya kilimo na hasa pembejeo za kilimo. Amesema kuwa Mkoa wa Iringa umepokea pembejeo za kilimo zenye thamani ya Shs. Bilioni 21.6. Amesema kuwa lengo la Serikali kuwekeza fedha nyingi katika pembejeo za kilimo ni kuboresha kilimo katika Mkoa wa Iringa ili kiwe ni kilimo chenye tija. Aidha, alikemea tabia ya ukiukwaji wa taratibu katika zoezi zima la ugawaji wa pembejeo hizo na kusema kuwa ukiukwaji hou umekuwa ukichelewesha shughuli za kilimo.
No comments:
Post a Comment