Serikali imewekeza zaidi ya shilingi Bilioni 21 kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo ili kiwe chenye tija na kuchangia zaidi katika pato la taifa mkoani Iringa.
Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kanali Mstaafu, Issa (RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Kanali Machibya amesema “Mkoa wa Iringa umepokea vocha za pembejeo za kilimo mbegu bora, mbolea ya kupandia na kukuzia zenye thamani ya shilingi Bilioni 21.6”. Ameelezea lengo la serikali kuwa ni kuboresha kilimo ili kiwe cha kisasa na chenye tija ili kichangie zaidi katika pato la Taifa.
Machibya hakusita kukemea vikali ukiukwaji wa taratibu na maadili katika zoezi la usambazaji wa vocha za pembejeo hali inayosababisha ucheleweshaji wa kilimo. Aidha, amewataka watendaji wote kuwajibika katika usimamizi na uratibu ili kuhakikisha wizi wa vocha za mbolea na mbegu na ukiukwaji wa tarabitu vitokomee.
Akielezea Mkoa ulivyojipanga kukabiliana na changamoto hizo, Katibu Tawala Msaidizi, Sehemu ya Sekta ya Uzalishaji Mali wa Sekretarieti ya Mkoa, Adam Swai amesema kuwa Wilaya zimeagiza wataalam wa kilimo katika ngazi zote kufuatilia zoezi la vocha pindi wanapofuatilia shughuli mbalimbali za kilimo vijijini.
Ameutaja mkakati mwingine kuwa ni muongozo wa utaratibu wa usambazaji wa ruzuku umefikishwa katika Halmashauri zote na waratibu wa pembejeo ngazi ya Mkoa na Halmashauri wametoa mfumo madhubuti wa mawasiliano ili kurahisisha uratibu wa zoezi hilo.
Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mikoa 20 (wilaya 87) inayotekeleza mpango wa Taifa wa kutoa ruzuku za pembejeo za kilimo yaani mbegu bora, mbolea ya kupandia na kukuzia. Aidha, mkoa una jumla ya 514 wanaosambaza pembejeo za kilimo. Vocha za ruzuku ya pembejeo za kilimo zilizotolewa na Serikali kwa mkoa wa Iringa ni vocha za kutosha Kaya 336,635 (sawa na vocha 1,009,905 kwa ujumla wa nakala moja moja ya vocha) na vocha hizi zinatosheleza ekari 336,635 kwa kufuata mwongozo wa ruzuku ya mbolea ya kupandia, mbegu na mbolea ya kukuzia kwa ekari moja kila mkulima.
No comments:
Post a Comment