Zaidi ya asilimia 70 ya matumizi ya kawaida ya Serikali ni kwa ununuzi wa bidhaa, huduma na malipo kwa kazi za ujenzi wa miundombinu.
Akiwasilisha mada juu ya Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2004, Uwezo wa Bajeti katika kufanikisha Manunuzi na Udhibiti wa Rushwa katika Manunuzi, Afisa Ugavi Msaidizi Mkoa wa Iringa, Janeth Kitinye amesema kuwa eneo la Manunuzi ya Umma ni muhimu sana kwa sababu hutumia sehemu kubwa ya fedha za walipa kodi wa Tanzania .
Bi. Janeth Kitinye, Afisa Ugavi Msaidizi Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa akiwasilisha mada
Aidha, ufanisi katika eneo hili ni chachu ya kufikia baadhi ya malengo makubwa ya kiuchumi na kijamii ya Taifa.
Amesema kuwa ukiondoa mishahara ya watumishi wa Serikali, karibu asilimia 70 ya Matumizi ya kawaida ya Serikali ni Ununuzi wa bidhaa, huduma na malipo kwa kazi mbalimbali. Vilevile, amesema karibu asilimia 100 ya matumizi ya Maendeleo ni kwa ajili ya ununuzi wa bidhaa, huduma na malipo kwa ajili ya kazi za ujenzi wa miudombinu na miradi mingine ya Maendeleo.
Amewataka watumishi wa Umma kuona kuwa wanalo jukumu kubwa la kuhakikisha Manunuzi wanayoyafanya yanawawezesha kupata bidhaa na huduma zenye Ubora kulingana na thamani ya fedha zilizotumika.
Kitinye amesema Sheria ya Manunuzi ya Umma ya Mwaka 2004, na Kanuni zake za Mwaka 2005 kwa pamoja zinaweka misingi na taratibu za kweza kufikia adhima hiyo.
Ameongoza kuwa Vitengo vya Manunuzi Vinajukumu la msingi la kuhakikisha kuwa huduma muhimu zinawafikia watumishi wa Umma na Wahitaji wengine katika muda uliopangwa na katika ubora unaokubalika. Sharia ya Manunuzi ya Mwaka 2004 na Kanuni zake za Mwaka 2005 zinawapngoza Watumishi wa Umma katika misingi ya Utawala Bora na uwajibikaji kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment