Serikali
imepongeza ushirikiano uliopo baina ya wananchi wa kijiji cha makungu na
muwekezaji wa kiwanda cha karatasi cha Mgololo (MPM) katika kuchangia maendeleo
ya wananchi.
Pongezi hazi
amezitoa Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma alipozindua mradi wa
maji wa kijiji cha Makungu uliofadhiliwa na kiwanda cha karatasi cha Mgololo
wilayani Mufindi.
Dkt. Christine
amesema “ushirikiano baina
ya muwekezaji kiwanda cha karatasi cha Mgololo na wananchi ni jambo la
kupongezwa sana
katika kusogeza huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi”. Amesema “mtu
anayekupa maji anakupa uhai hivyo mnawajibu wa kutunza na kulinda miundombinu
hii ya maji ili muweze kujihakikishia wahakika wa maji na kuufanya mradi huu
kuwa endelevu”. Aidha, ametoa wito kwa wawekezaji wengine kuona kuwa wanawajibu
wa kuisaidia jamii inayowazunguka kwa kufadhili miradi nashuighuli za kijamii
ili kudumisha ushirikiano na uhusiano mwema.
Katika taarifa ya
kijiji iliyowasilishwa na Afisa Mtendaji wa kijiji Ephaim Mhelela amesema kuwa
kijiji kupata mradi huo kimefanikiwa kupunguza tatizo la maji kutokana na kuwa
na bomba moja tu la maji
lililokuwa katika kitongoji kimoja kabla ya mradi huo.
Amezitaja
changamoto katika mradi huo kuwa ni pamoja na ukubwa wa eneo la kijiji jambo
linalofanya baadhi ya vitongoji visifikiwe kwa urahisi kutokana na umbali. Changamoto
nyingine ameitaja kuwa ni maji kutotosheleza kwa watumiaji wote waliofungiwa
bomba kutokana na uchache wa naji yanayopatikana katika tenki na ukosefu wa
fedha za kuendeshea mradi ili huduma hiyo iwafikie wananchi wote.
Aidha, ameitaja
baadhi ya mikakati ya kukabiliana na changamoto hizo kuwa ni pamoja na kutumia
nguvu kazi ya wananchikwa kuchimba mitaro ya maji pindi pale bomba
zinapopatikana za kusambaza maji na kuanzisha mfuko wa maji kwa kuwachangisha
wananchi wenyewe.
Mradi huo wa maji
unahudumia kijiji cha Makungu chenye vitongoji saba na idadi ya kaya 1,445 na
wakazi 6,125, wakiwepo wanawake 3,230 na wanaume 2,895. aidha jumla ya watu
wenye uwezo wa kufanya kazi ni 3202.
=30=
No comments:
Post a Comment