Ujangili na uharibifu wa mazingira vinachangia sana kupunguza
idadi ya tembo duniani na hasa Tanzania kutokana na tembo wengi kuuliwa na
kusababisha kuathiri utalii na baadhi ya spishi za wanyamapori kuwa hatarini kupotea.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii,
Lazaro Nyalandu katika mkutano wa wadau wa mtandao wa kuboresha ulinzi wa
maeneo ya hifadhi kusini mwa Tanzania uliofanyika katika ukumbi wa Siasa ni
Kilimo Wilaya ya Iringa.
Nyalandu amesema kuwa tafiti zinaonesha kuwa ujangili na
uharibifu wa mazingira kwa pamoja vimechangia kupungua kwa idadi ya tembo
dunia. Amesema kuwa kwa mujibu wa takwimu za mwaka 1930 kulikuwepo na tembo milioni
50 na sasa wamepungua na kubaki tembo 402,067 tu. Amesema kuwa ujangili huo
unahatarisha kupotea kwa tembo na baadhi ya spishi za wanyamapori zinazotegemea
wcolojia waliopo tembo. Amesema kuwa ugangili huo unaathiri utalii pia.
Naibu waziri wa maliasili amesema kuwa hali hiyo inaashiria
kutokuwepo kwa amani na usalama katika hifadhi na uchumi wa nchi. Amesema athari
ya kiuchumi ni kubwa kwa sababu ujangili unaathiri uchumi kwa sababu idadi ya
watalii wanaotembelea inapungua na hatimae kupunguza pato la taifa. Amesema kuwa
ujangili unaathiri sana uchumi wan chi kwa sababu asilimia 17 ya pato la taifa
linategemea utalii.
Akiongelea mbinu za
kukabiliana na mtandao wa ujangili unaotumia silaha za kisasa, amesema vi vema
kuongeza uwezo wa kukabiliana na njama zinazotishia kupotea kwa tembo katika
sura ya dunia. Aidha, ameutaka mkutano huo kujadili kwa kina kutoka na ufumbuzi
wa changamoto zinazoikabili sekta ya ulinzi wa rasilimali za wanyamapori hasa
tembo.
Akielezea malengo ya mkutano huo, mratibu wa mradi wa kuboresha mtandao
wa maeneo ya hifadhi kusini mwa Tanzania (SPANEST) ambao pia ni waandaaji wa
mkutano huo, Godwell Ole Meing’ataki ameyataja malengo kuwa ni kutoa fursa kwa
wadau na viongozi wa ngazi mbalimbali katika mikoa ya nyanda za juu kusini kubadilishana
uzoefu, mbinu na mikakati ya kuboresha shughuli za uhifadhi katika mikoa ya nyanda
za juu kusini. Lengo jingine amelitaja kuwa ni Kuweka mikakati ya kukabiliana
na wimbi la ujangili wa tembo kwa kushirikisha wadau mbalimbali kwa kutambua
kuwa hakuna mamlaka moja au mdau ambaye anaweza kukabiliana na janga hili bila
ya ushirikiano wa wadau wengine pamoja na Kujadili kwa undani juu ya wimbi la ujangili
wa tembo katika maeneo ya hifadhi na mapori ya wanyamapori katika maeneo ya nyanda
za juu kusini na nchi kwa ujumla.
=30=
No comments:
Post a Comment