HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA NA MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI TAIFA KATIKA
SHEREHE ZA KUTIMIZA MIAKA 37 YA UHAI WA CCM KWENYE UWANJA WA SOKOINE, MBEYA,
TAREHE 2 FEBRUARI, 2014
Ndugu Philip Mangula, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara,
Ndugu
Godfrey Zambi, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Mbeya na Naibu Waziri wa Kilimo,
Chakula na Ushirika,
Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM
Taifa,
Ndugu Wajumbe wa Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya
Taifa,
Ndugu Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya
Taifa Mliopo,
Watendaji Wakuu wa Serikali na viongozi wa CCM wa Ngazi
Mbalimbali,
Wanachama Wenzangu wa CCM,
Mabibi na
Mabwana
Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, mwingi wa
rehema, kwa kutujaalia uzima na kutuwezesha
kukutana siku ya leo hapa Mbeya, kuadhimisha
miaka 37 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi. Nawashukuru sana viongozi,
wanaCCM na wakazi wote wa Mbeya kwa mapokezi mazuri na ukarimu wenu kwangu na
wageni wenzangu tangu tulipowasili jijini hapa jana mpaka sasa.
Wakika tutaondoka Mbeya tukiwa na
kumbukumbu nzuri ya ukarimu na upendo wenu kwetu.!hukrani nyingine nazitoa kwa viongozi na wanachama
wenzetu wa Mbeya kwa kukubali kuwa
mwenyeji wa sherehe hizi. Nafahamu fika kwamba kuandaa sherehe kubwa kama hii si jambo jepesi.
Lakini, inafurahisha na kuleta
faraja kwamba, kutokana na moyo wenu wa kujitolea, umahiri na umakini wenu, mambo yamefana sana.
|
Mwenyekiti wa CCM (T) Rais Jakaya Kikweye akihutubia mamia ya wananchi njini Mbeya |
Matembezi ya mshikamano yalifana sana na hapa kiwanjani mambo ni
mazuri sana. ongereni sana. Niruhusuni, kupitia hadhara hii,
niwapongeze kwa dhati viongozi, wanachama,
makada, wapenzi na washabiki wote wa CCM kote nchini kwa kuadhimisha miaka 37 ya uhai wa Chama chetu.
Tunafanya sherehe hizi leo kwa
vile tarehe 5 Februari, 2014 ni siku ya kazi.
Si vyema kuwatoa watu kazini. Ndiyo maana tunafanya madhimisho
haya leo. Tunayo kila sababu ya kusherehekea siku hii kwa vifijo
na nderemo kama tufanyavyo siku zote. ii ni kutokana na ukweli kuwa CCM ina historia iliyotukuka, kuvutia na kusisimua.
Chama chetu kimepata mafanikio makubwa tangu kuasisiwa kwake tarehe 2 Februari, 1977 mpaka sasa.
Tumefanya mambo mengi mazuri kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake. Nchi
imetulia, kuna amani na utulivu na maendeleo ya kichumi na kijamii yanazidi kupatikana kila kukicha. Mwenye macho haambiwi
tazama. Ni jambo linalourahisha na kutia moyo na, la kujipongeza
kwa kipindi cha miaka 37 kati ya hiyo
ikiwa ndani ya mfumo wa vyama vingi, CCM imeendelea kuwa Chama kikubwa na chenye nguvu kuliko vyama vyote hapa nchini.
Aidha, CCM imebaki kuwa chama chenye
mafanikio makubwa na kukubalika zaidi na Tatanzania kuliko vyote kwa
kila hali na kwa vigezo vyote. Japo
wanaojaribu kuiga lakini hawajaweza.
Kwa kweli, itawachukua miaka mingi kufikia hata theluthi moja ya
hapa tulipofikia sisi. CCM inaongoza na wengine wanafuatia.
Ninyi na mini tunavifahamu vyama kadhaa vya siasa ambavyo vilianzishwa lakini havijapata mafanikio
kama Chama chetu na baadhi havikudumu.
Baadhi ya vyama na watu walijifanya bundi na kukitabiria kifo Chama cha Mapinduzi. Nilisema wakati ule kuwa
CCM haifi na si ajabu vitakufa
vyama vyao na CCM wataiacha hapa hapa. Haya kiko wapi CCM ipo haipo? CCM hai
siyo hai? CCM ipo, CCM ni hai na wala haina dalili ya ugonjwa wo wote. Wahenga walisema dua la kuku
halimpati mwewe na mchimba shimo
hujichimbia mwenyewe. /aadhi yao sasa wanahangaika nchi nzima wakitapatapa kujinusuru. Tanakabiliwa na
migogoro mikubwa inayotishia uhai wao. Lakini, sisi hatuwaombei
mabaya.
Ndugu WanaCCM Wenzangu"
Pamoja na ukweli kwamba Chama cha Mapinduzi
ni kikubwa, kina nguvu na kimepata ma"aniko makubwa tusije tukalewa
mafanikio na kujisahau hata mara
moja. Wenzetu wanaendelea kujijenga na wanapata mafanikio ya kiasi
chao. Hivyo basi, lazima tuendelee kufanya kazi ya kuimarisha Chama ili kiendelee na hata kizidi kukua na kuwa na nguvu
kubwa zaidi. Mtakumbuka kuwa,
4ktoba, '((5 tulianzsha Mradi wa uimarisha Chama kwa lengo la kuelekeza na kuongoza shughuli ya kuimarisha
Chama cha Mapinduzi. uu ni mradi
wa tatu katika historia ya CCM. Lazima tufanye kila tuwezalo kuhakikisha kuwa malengo na madhumuni ya Mradi
huo yanatekelezwa kwa ukamilifu. atuna budi kutambua kuwa uhai na maendeleo
ya CCM sasa na kwa miaka mingi ijayo yatategemea ufanisi wetu katika
utekelezaji wa Mradi wa Tatu wa uimarisha Chama.
Ndugu (iongozi na WanaCCM"
Kwa sababu ya Uchaguzi wa !erikali za Mitaa
mwaka huu na Uchaguzi Mkuu mwakani kazi ya kuimarisha Chama cha
Mapinduzi ina umuhimu wa kipekee. Lazima tupate mafanikio katika
jambo hilo kwani yanakipa Chama chetu nguvu ya kutuwezesha kupambana na
kupata ushindi katika chaguzi hizo. azi nzuri tuliyo"anya katika
utekelezaji wa mradi wa kuimarisha Chama miaka iliyopita ndiyo iliyotupa mafanikio makubwa. Hivyo basi tukifanya vizuri mwaka huu
tutapata ushindi kama ule au hata zaidi. Bila
shaka sote tunatambua kuwa kazi ya kuimarisha Chama inahusisha mambo matatu wanza, kujenga na kuimarisha Chama
kama taasisi. ili kufanya kazi
ya Chama ndani ya umma. Na tatu ni kufanya kazi ya kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama, sera
na maamuzi ya Chama unaofanywa na Serikali na vyombo vyake. Naamini wote
mnajua kuwa sizungumzii mambo
mapya. Mambo yote matatu tunayajua kwani tumekuwa tunayafanya kwa miaka
mingi. Ninachokifanya leo ni kukumbushana juu ya umuhimu wa kuendelea
kufanya kazi hiyo ila tuifanye kwa ufanisi zaidi, kwa nguvu
zaidi, ari zaidi na kasi zaidi.
Ndugu (iongozi Wenzangu"
Jambo
la kwanza muhimu kwetu kufanya ni kuona kuwa viungo vyote vya
Chama chetu viko kamilifu na vinafanya kazi vizuri. Chama kiwe na wanachama
wengi ambao wanatimiza ipasavyo wajibu wao kwa Chama chao. Viongozi
wa Chama wawe hodari kufanya kazi ndani ya Chama na ndani ya umma.
Tasiwe mangimeza bali watoke waende kwa wanachama kuimarisha uhai wa Chama.
Tuaende kwa wananchi kukisemea Chama, kusikiliza shida zao na kusaidia
kutafuta ufumbuzi. Lazima Chama kiwe mlezi na kimbilio la wananchi.
Tukifanya hivyo watu wetu watakuwa na imani na mapenzi na CCM
hivyo watakiunga mkono katika chaguzi za dola. Tuhakikishe kuwa
vikao vinafanyika ipasavyo kwani vikao
ndiyo msingi mkuu wa demokrasia ndani ya Chama. Maamuzi ya
Chama hufanywa na vikao siyo kiongozi peke yake.
Lazima pia Chama kiwe na uwezo wa rasilimali Fedha na vifaa ili viongozi
na wanachama waweze kufanya kwa ufanisi kazi ya Chama ndani ya Chama na nje ya Chama na
ndani ya umma. Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha agizo letu
la siku nyingi la kila ngazi ya Chama kuwa
na shughuli za kuwaingizia mapato na kuw ana Mfuko wa Uchaguzi. Maagizo haya hayajatekelezwa ipasavyo kote nchini. Uhodari wa uongozi hupimwa kwenye matatizo.
Lazima viongozi wa
CCM tuwe wabunifu ili tulipatie jawabu endelevu, tatizo la ukwasi
hasi. Tatizo linalohatarisha murua wa
Chama cha Mapinduzi kwani baadhi ya viongozi na wanachama sasa hawachagui
nani anachangia Chama. Tunachukua hata mtu mwenye pesa chafu au
wenye nia chafu. ata wanaotoa rushwa nao hupokewa kishujaa badala ya
kuwanyanyapaa na kuwaweka mbali nasi. Jambo
lingine muhimu kuhusu kuimarisha CCM kama taaasisi ni kuwa na Jumuiya zilizo imara ili kukiongezea Chama
wanachama, wapenzi na washabiki wa kukiunga mkono wakati wote na hasa wakati
wa uchaguzi. Jambo la mwisho kubwa
na muhimu ni kuwepo umoja na mshikamano miongoni mwa viongozi kwa viongozi, wanachama kwa wanachama na baina ya viongozi na wanachama. Hii ndiyo silaha ya
kuangamiza adui na kujihakikishia
ushindi. Unapokosekana umoja na mshikamano, adui hupata nafasi ya kupenya. Ndiyo maana wakati mwingine
hata pale tusipostahili kushindwa
tunashindwa. Hivyo tuzingatie na kutekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya
CCM ya Umoja ni Ushindi.
Ndugu viongozi na Ndugu Wanahama
Uwezo na sifa ya
Chama cha Mapinduzi kupata ushindi kunategemea pia taswira yake katika jamii. Kama taswira yake ni nzuri Chama hukubalika
kwa watu hivyo wanakuwa tayari
kukiunga mkono.
Kama taswira ya Chama ni mbaya watu hukichukia na hukataa kukiunga mkono. Katika mazingira hayo
kushindwa huwa ni dhahiri. 8li mpate ushindi mnalazimika kufanya kazi ya
ziada na kutumia nguvu kubwa mno.
Aghalabu, ushindi wenyewe huwa mwembamba. !era nzuri za CCM, utendaji
mzuri wa Serikali zake na matendo mema na tabia njema za viongozi na wanaCCM
hujenga mapenzi ya jamii kwa Chama na hivyo kuungwa mkono. Sera mbaya,
utekelezaji mbaya wa Serikali, vitendo vya
rushwa, wizi na ubadhilifu huondoa mapenzi ya wananchi kwa Chama. Kuzaa chuki na hupunguza kuungwa mkono na
kuhatarisha ushindi. Lazima wakati wote tuhakikishe kuwa taswira ya Chama
chetu mbele za watu ni nzuri. Watu
wote na mambo yote ambayo yatakuwa kinyume
|
No comments:
Post a Comment