Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM),Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono baadhi ya Wananchi (hawapo pichani),walioshirikia matembezi ya mshikamano yaliyoanzia viwanja vya Soweto,kuelekea kwenye bustani iliyopo nje ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya mapema leo asubuhi,ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya kusherehekea miaka 37 kuzaliwa kwa chama cha CCM.Kushoto kati ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mbozi Mashariki,Mh.Godfrey Zambi,Katibu Mkuu wa chama hicho,ndugu Kinana pamoja na Katibu wa Uchumi na Fedha,Bi Zakia Meghji wakishiriki matembezii hayo yaliyofana kwa kiasi kikubwa jijini humo.Rais Kikwete ambaye ndiye mgeni rasmi wa sherehe hizo atahutubia leo mchana kwenye maadhimisho ya sherehe hizo zitakazofanyika katika uwanja wa Sokoine mkoani humo. |
No comments:
Post a Comment