Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa IRINGA
Kliniki
maalumu ya kupima ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu mkoani Iringa imevuka
lengo kwa kufanikiwa kupima wananchi zaidi ya 2,000.
Kauli
hiyo ilitolewa na Mganga mkuu wa mkoa wa Iringa Dkt Robert Salim alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari katika hitimisho la siku tano za kliniki hiyo iliyofanyika
katika viwanja vya bustani ya Manispaa mjini Iringa.
Dkt.
Salim alisema “kliniki ya kupima ugonjwa wa kisukari na shinikizo la damu
imefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Tumefanikiwa kuwapima wananchi 2,007 na kuvuka
lengo letu la kuwapima wananchi 2,000, hivyo lengo limefikiwa kwa asilimia
100.35”. Alisema kuwa mafanikio haya yanatokana na utayari wa wananchi wa mkoa
wa Iringa kujitokeza kupima afya zao pindi fursa zinapojitokeza za upimaji
zinapojitokeza.
Mganga
mkuu wa mkoa aliwataka waratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika
halmashauri kuanzisha kliniki za magonjwa yasiyo ya kuambukiza katika
halmashauri zao na kutoa huduma za mkoba. Aidha, liwataka kufikiria kuanzisha
utaratibu wa kuwapima watumishi katika taasisi mbalimbali ili kuwapa fursa ya
kunufaika na huduma za afya kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza.
Dkt
Salim aliwatka wananchi wa mkoa wa Iringa kujikita katika kufanya mazoezi kama
kutembea na kukimbia ili kujikinga na kisukari. Rai nyingine alitoa kuwa
wananchi kuacha tabia ya kula vyakula vyenye mafuta, kupunguza unywaji wa pombe
kupita kiasi na uvutaji wa sigara.
Akiongelea
ufanisi wa kliniki hiyo, Dtk Tatu Mbotoni wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa
alisema kuwa kliniki hiyo ilifanikiwa kutokana na timu yake ya wataalam
kujipanga vizuri kuwahudumia wananchi wote waliojitokeza kwa muda. “Tulipanga
timu ya wataalam wa kutosha kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa na hospitali ya
manispaa Frelimo.
Lengo
la kuandaa wataalam wengi ni kuhakikisha kila mwananchi anayehudhuria
anahudumiwa haraka sana ili aweze kuendelea na mjukumu yake tukizingatia
matakwa ya serikali ya awamu ya tano ya hapa kazi tu’’ alisema Dkt Mbotoni.
Nae
Elimina Sanga aliyefika katika kliniki hiyo, alisema ameridhishwa na huduma
alizopata na kuomba kliniki hiyo iwe endelevu badala ya kusubiri kwenye
maadhimisho ya siku ya kisukari duniani.
=30=
No comments:
Post a Comment