Na Dennis Gondwe, IRINGA
Halmashauri
za mikoa ya nyanda za juu kusini zatakiwa kushiriki kikamilifu maonesho ya
utalii karibu kusini ili kutangaza fursa za utalii na viwanda vidogo vilivyopo
maeneo yao.
Kauli
hiyi ilitolewa na waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa afrika mashariki,
kikanda na kimataifa Dr. Augustino Mahiga alipokuwa akifunga maadhimisho ya siku
ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya
wajasiriamali wa viwanda vidogo nyanda za juu kusini yaliyofanyika mjini
Iringa.
Dr.
Mahiga alisema “natoa wito kwa
halmashauri zote na wadau katika mikoa ya nyanda za juu kusini kuanza kujiandaa
kikamilifu kushiriki katika maonesho haya ili kutumia nafasi hii kujitangaza na
kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii na viwanda”.
Waziri huyo
aliwataka SIDO kufanya kazi kwa kujituma ili wajasiriamali waliojitokeza
wabadilike na kuwa wafanyabiashara wakubwa. Aliongeza kuwaa wjasiriamali
watakapobadilika na kuwa wafanya biashara wakubwa waendelee kuwasaidia wajasiriamali
wengine ili wakue.
Dr.
Mahiga alielezea matumaini yake kuwa maonesho ya mwaka 2018 yatakuwa yenye
ufanisi mkubwa kwa kushirikisha wadau wengi kutoka sehemu mbalimbali za nchi na
nchi jirani.
“Tuzingatie tu kuwa utalii
hauna mipaka na ni vema sasa tuanze kujitangaza pia kwa nchi jirani za Zambia,
Malawi, Msumbiji, na hata Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na kutumia
balozi zetu za nje” alisema Dr. Mahiga.
Maadhimisho
ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya shughuli
za wajasiriamali wa SIDO yamehusisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma, Rukwa,
Songwe, Mwanza, Pwani, Dar es Salaam, Geita, Lindi, Morogoro, Kilimanjaro, Tabora na nchi
ya Kenya. Maonesho hayo yamehusisha mashine mbalimbali, bidhaa za usindikaji,
bidhaa zilizosindikwa, bidhaa za ngozi, kazi za mikono na dawa.
=30=
No comments:
Post a Comment