Na Dennis Gondwe, IRINGA
Wajasiriamali
wengi wanakabiliwa na tatizo la kujitangaza jambo linalosababisha washindwe
kufikia masoko ya bidhaa kwa urahisi.
Kauli
hiyo ilitolewa na meneja wa SIDO Mkoa wa Ruvuma, Martin Chang’a alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari waliotembelea banda la SIDO katika maadhimisho
ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya
shughuli za viwanda vidogo (SIDO) kwa mikoa ya nyanda za juu kusini
yaliyofanyika mkoani Iringa hivi karibuni.
Chang’a
alisema kuwa wajasiriamali wengi wanajuhudi ya kuzalisha bidhaa nzuri kutokana
na mafunzo wanayoyapata kutoka SIDO, changamoto ni jinsi ya kufikia masoko.
Alisema kuwa tatizo kubwa linalowakabili wajasiriamali ni mbinu za kujitangaza
na kutangaza bidhaa zao.
“Mbinu za
kujitangaza ni muhimu sana kwa wajasiriamali kwa sababu zinawasaidia katika
kufikia masoko kirahisi. Kwa kuona tatizo hilo, SIDO tumetoa mafunzo ya jinsi
ya kuboresha mbinu za kujitangaza kwa wajasiriamali wanaoshiriki maonesho haya
ili kuwasaidia kuwa na uwezo wa kujitangaza” alisema Chang’a.
Akiongelea
lengo la maonesho hayo kwa upande wa SIDO, Meneja wa SIDO mkoa wa Ruvuma
alisema kuwa maonesho hayo yanalenga kuwatangaza wajasiriamali na shughuli
wanazofanya ili zijulikane kwa watu. Aliongeza kuwa, maonesho hayo yanawawezesha
wajasiriamali kukutana na kubadilishana uzoefu katika shughuli zao.
Maadhimisho
ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya
shughuli za wajasiriamali wa SIDO yamehusisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma,
Rukwa, Songwe, Mwanza, Pwani, Dsm, Geita, Lindi, Morogoro, Kilimanjaro, Tabora
na nchi ya Kenya. Maonesho hayo yamehusisha mashine mbalimbali, bidhaa za
usindikaji, bidhaa zilizosindikwa, bidhaa za ngozi, kazi za mikono na dawa.
=30=
No comments:
Post a Comment