Na Dennis Gondwe, IRINGA
Maadhimisho
ya siku ya utalii ya utalii duniani, maonesho ya karibu kusini na maonesho ya
wajasiriamali wa viwanda vidogo mikoa ya nyanda za juu kusini yamefanikiwa
kutoa elimu ya ujasiriamali na utalii.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza katika salamu zake
wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii
karibu kusini na maonesho ya shughuli za wajasiriamali wa wa viwanda vidogo wa
mikoa ya nyanda za juu kusini yaliyofanyika mkoani Iringa jana.
Masenza
alisema kuwa maonesho hayo yamekuwa ya manufaa kwa jamii. “Maonesho haya yametoa elimu ya masuala ya utalii na ujasiriamali, ajira
kwa watoa huduma mbalimbali wakati wa maonesho na washiriki wameweza
kubadilishana uzoefu na kupata masoko ya bidhaa” alisema Masenza.
Mafanikio
mengine, mkuu wa mkoa wa Iringa aliyataja kuwa ni kuongezeka kwa wadau wanaotaka
kuwekeza katika mikoa ya nyanda za juu kusini.
Masenza alisemaa kuwa maonesho ya karibu
kusini mwaka 2017 yalijumuisha maeneo sita ikilinganishwa na maeneo matatu ya
mwaka 2016. Aliyataja maeneo hayo kuwa ni ziara za kutembelea hifadhi ya Taifa
ya Ruaha pamoja na baadhi ya vivutio, maonesho ya wanyama hai, maonesho ya
ngoma za asili, kongamano la utalii endelevu na uendeshaji viwanda kwa mikoa ya
nyanda za juu kusini na maonesho kwenye mabanda kwa kuonesha bidhaa za
wajasiriamali wa viwanda vidogo na watoa huduma za utalii.
Maadhimisho
ya siku ya utalii duniani, maonesho ya utalii karibu kusini na maonesho ya
shughuli za wajasiriamali wa SIDO yamehusisha mikoa ya Iringa, Njombe, Ruvuma,
Rukwa, Songwe, Mwanza, Pwani, Dar es Salaam, Geita, Lindi, Morogoro,
Kilimanjaro, Tabora na nchi ya Kenya. Maonesho hayo yamehusisha mashine
mbalimbali, bidhaa za usindikaji, bidhaa zilizosindikwa, bidhaa za ngozi, kazi
za mikono na dawa.
=30=
No comments:
Post a Comment