Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-IRINGA
Wakulima
mkoani Iringa washauriwa kuzitumia vizuri mvua zilizoanza kunyesha kupanda kwa
kutumia mbegu bora na kuzingatia mistari.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa mkoa wa Iringa, mheshimiwa Amina Masenza alipokuwa
akiongea katika kipindi cha moja kwa moja cha Sunrise power kinachorushwa na
kituo cha redio Nuru cha mjini Iringa jana.
Mheshimiwa
Masenza alisema kuwa mvua zilizoanza kunyesha zitumike vizuri kwa kupandia. Aliwataka
wakulima kuchagua mbegu bora zilizoidhinishwa na wataalam ili waweze kupata
mazao bora. Aidha, alishauri kufuata ushauri wa wataalam wa akilimo ili kupata
tija kupitia kilimo.
Mkoa
wa Iringa ni miongoni mwa mikoa iliyo mstari wa mbele katika kilimo cha mazao
ya chakula katika mikoa ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania.
=30=
No comments:
Post a Comment