Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Mkoa
wa Iringa unatumia mkakati wa maonesho ya utalii karibu kusini kuchochea na
kukuza utalii kwa ukanda wa kusini mwa Tanzania.
Kauli
hiyo ilitolewa na mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza alipokuwa akisoma
taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Iringa kwa Makamu wa Rais katika rest house ya
NSSF Iringa mjini jana.
Masenza
alisema “maonesho ya utalii kusini yanatumika kama mkakati maalum wa kufungua
sekta ya utalii kwa ukanda wa kusini ambao umejaa fursa na vivutio vya kipee
katika utalii. Mkoa wa Iringa ukiwa mratibu umeandaa mipango ya kuboresha wa
maonesho haya kwa kutenga eneo la Kihesa Kilolo kama eneo maalum kwa ajili ya
maonesho ya utalii kusini. Eneo hili litatumiwa na wadau wa utalii na wadau wa
maendeleo kujenga miundombinu kwa ajili ya kuonesha huduma na bidhaa za sekta
ya utalii”.
Idadi
ya watalii waliotembelea vivutio vya utalii kwa mwaka 2015 walikuwa 8,112 kati
ya hao watalii wa nje walikuwa 6,875 na watalii wa ndani walikuwa 3,072. Kwa
mwaka 2016 jumla ya watalii 36,736 kati ya watalii hao watalii wa ndani
walikuwa 22,280 na watalii wa nje walikuwa 14,456 alisema mkuu wa Mkoa.
Aidha,
Mkoa kwa kushirikiana na wadau unaendelea kuvihifadhi na kuvitangaza vivutio
hivyo ili kukuza utalii. Alisema kuwa Mkoa wa Iringa ambao ni kitovu cha utalii
kwa mikoa ya nyanda za juu kusini umeweza kuratibu kwa kuandaa maonesho ya
utalii karibu kusini kwa miaka miwili mfululizo (mwaka 2016 na mwaka 2017).
Maonesho
ya utalii karibu kusini hushirikisha mikoa ya nyanda za juu kusini ambayo ni
Iringa, Njombe, Mbeya, Ruvuma, Songwe, Rukwa na Katavi.
Makamu
wa Rais yupo katika ziara ya siku tano mkoani Iringa pamoja na mambo mengine
atazingua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini REGROW.
=30=
No comments:
Post a Comment