Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Taasisi ya kuzuia na
kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Iringa imetakiwa
kuhakikisha rushwa inakuwa historia mkoani hapa kwa kushughulikia taarifa za malalamiko
ya rushwa kutoka kwa wananchi ili waendelee kuwa na Imani na taasisi hiyo.
Rai
hiyo imetolewa na mkurugenzi mkuu wa NSSF, Prof. Godius Kahyararavalipotembelea
banda la TAKUKURU katika maonesho ya shughuli na huduma za wafanyakazi
yanayoendelea katika uwanja wa Kichangani mjini Iringa jana.
Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Prof. Kahyarara alipotembelea banda la TAKUKURU Iringa |
Prof.
Kahyarara alisema kuwa TAKUKURU ina wajibu wa kuhakikisha rushwa inakomeshwa
mkoani Iringa ili wananchi waweze watekeleza majukumu yao. Alisema kuwa rushwa
imekuwa ikikwamisha maendeleo ya wananchi na kuwanyima haki ya kupata huduma.
“TAKUKURU mnawajibu wa kuifanya Iringa kuwa eneo huru dhidi ya rushwa. Na huu
ndiyo wajibu wenu wa msingi” alisema Prof. Kahyarara.
Awali
afisa muelimishaji wa TAKUKURU mkoa wa Iringa, Aneth Mwakatobe alieleza kuwa
hali ya rushwa mkoani Iringa imeendelea kushuka katika miaka ya hivi karibuni.
Alisema kuwa hali ya rushwa imeendelea kushuka mkoani hapa kutokana na uelewa
wa wananchi kuwa mkubwa.
“TAKUKURU mkoa
wa Iringa imekuwa ikitoa elimu kwa wananchi kuhusiana na jinsi ya kukabiliana
na rushwa. Katika kuonesha uelewa mkubwa kwa wananchi, wananchi wameendelea
kutoa taarifa kwetu na kusaidia uchunguzi kufanyika na kutoa matokea chanya”
alisema Mwakatobe.
Afisa
huyo aliyataja maeneo yanayolalamikiwa kuwa na vitendo vingi vya rushwa ni yale
ambayo watoa huduma wake wanakutana na wananchi moja kwa moja. Alitolea mfano
wa maeneo hayo kuwa ni halmashauri, polisi, mahakama, ardhi, na afya.
TAKUKURU
ni moja ya waoneshaji wa huduma katika mabanda ya maonesho ya Mei Mosi kitaifa
yanayofanyika katika viwanja vya kichangani mjini Iringa yakitangulia sherehe
ya Mei Mosi kitaifa itakayohudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
=30=
No comments:
Post a Comment