Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Iringa
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Amina Masenza ameridhishwa na hali ya
maandalizi ya mabanda ya maonesho ya shughuli na huduma zinazofanywa na
wafanyazi nchini.
Akitoa hali ya tathmini ya mabanda ya
maonesho baada ya kuyatembelea jana jioni mbele ya waandishi wa habari katika
uwanja wa maonesho wa Kichangani, Masenza alisema kuwa ameridhishwa na hali ya
mabanda.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, akipokelewa na Meneja wa TTCL Iringa |
“Hadi sasa mabanda yamekwisha
pambwa vizuri na huduma na bidhaa mbalimbali zimeanza kuoneshwa mezani na
wananchi wakitembelea mabanda hayo makumi kwa mamia”. Aidha, alitoa rai kwa
wajasiriamali wa mkoa wa Iringa kuendelea kujitokeza kuonesha bidhaa zao kwa
sababu nafasi za mabanda bado zipo. Alisema maonesho ya bidhaa na huduma za
wanafanyakazi ni fursa nzuri kujitangaza na kutangaza huduma na bidhaa
zinazofanywa na wafanyakazi ndani na nje ya mkoa.
Mkuu wa mkoa amewataka wananchi wote
katika Manispaa ya Iringa na vitongoji vyake kujitokeza kwa wingi kutembelea
mabanda na kujionea bidhaa na huduma zinazooneshwa pamoja na kujifunza mambo
mbalimbali yanayohusu masuala afya na usalama mahala pa kazi. Alisema kuwa
maonesho hayo yatafunguliwa rasmi tarehe 27/4/2018.
Awali mkuu wa mkoa alitembelea uwanja
wa michezo wa Samora kuangalia ukarabati kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za
Mei Mosi, 2018.
Mkoa wa Iringa ni mwenyeji wa
maadhimisho ya siku ya wafanyakazi (Mei Mosi) kitaifa na mgeni rasmi atakuwa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
=30=
No comments:
Post a Comment