Tuesday, December 10, 2013

Dunia yaomboleza kifo cha Mandela




 6 Disemba, 2013 - Saa 17:22 GMT 

Mandela atazikwa tarehe 15 mwezi Disemba
Wananchi wamejitokeza katika sehemu nyingi za Afrika Kusini wakiomboleza kifo cha kiongozi wao Nelson Mandela Mandela.
Mji wa Johannesburg umemiminika watu waliojitokeza kumkumbuka Mandela na kutoa rambi rambi zao kwa jamii, familia na marafiki wao.
Viongozi duniani pia wameendelea kutuma rambirambi zao kufuatia kifo cha Mandela.
Kifo cha Mandela kilitangazwa hapo jana Alhamisi saa za usiku naye Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliyesema kuwa Afrika Kusini inaomboleza kumpoteza kiongozi huyo waliyemuenzi sana kama mtoto wao , baba yao na kiongozi wa taifa hilo.
Je uko Afrika Kusini? Unaweza kututumia picha au video kuhusu yanayojiri huko na tutayaweka hapa kwenye mtandao wetu. Tutumie picha au ujumbe wako wowote kupitia ukurasa wetu waFacebookbbcswahili
Mandela alifariki nyumbani kwake mjini Johanesburg na alikuwa ameugua homa ya mapau kwa muda mrefu.
Na wewe pia unaweza kutuma ujumbe wako kupitia ukurasa wetu wa Bofya Facebook ambao kisha nitauweka kwenye mtandao wa Bofya bbcswahili
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kuwa Mzee Mandela, miongoni mwa wengine kama Oliver Tambo, Govan Mbeki na wengine, walijitlea maisha yao na ujana wao wote katika kupigania haki na kuikomboa Afrika Kusini. Walijivunia kweli walichoamini na wakatekeleza. Sasa ni jukumu letu na wadogo wetu kuendeleza kazi ya Mandela.''
Rais wa Malawi Joyce Banda, "Wakati kama huu, sote tumepata mshtuko. Sio kuwa hatukujua kitatokea, lakini ni huzuni kwa tulichopoteza. Ningependa kuelezea masikitiko yangu kwa kumpoteza kijana wa Afrika Dr.
Nelson Mandela kwasababu vita alivyopigana sio tu dhidi ya ubaguzi wa rangi bali ni vita dhidi ya unyanyasaji wa aina yoyote dhidi ya binadamu.
Na ndio maana vijana, na wazee, wake kwa waume, weupe na weusi tajiri na masikini wote wamejihusisha na yeye na vitu alivyopigania."
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema kuwa Hayati Nelson Mandela atazikwa tarehe kumi na tano Jumapili mwezi Disemba katika eneo la Qunu mkoa wa Estern Cape.
Waziri mkuu wa India, Manmohan Singh, "Kifo cha mandela. Huyu alikuwa mwakilishi wa utu duniani.
Pia amekuwa chanzo cha matumaini kwa wengine wengi ambao wanakabiliana na unyanyasaji na kunyimwa haki, hata miaka yote hiyo baada ya kuwakomboa watu wake wenyewe.
Katika ulimwengu uliogubikwa na migawanyiko, amekuwa mfano mwema wa utangamano na sioni uwezekano wa kupatikana mwingine kama yeye katika miaka mingi ijayo."
@bbc.co.uk/swahili/habari/2013/12/131206_mandela_dunia_omboleza.shtml




Thursday, November 28, 2013

REVINA PIUS AHITIMU SHAHADA YA UZAMILI KATIKA UONGOZI WA BIASHARA RUCO


                            Maandamano ya kitaaluma kuelekea katika uwanja wa Mahafali

                      Revina Pius akiwa tayari kwa kuhudhurishwa na Mkuu wa Chuo kikuu cha Ruaha

                   Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara tarari kuhudhurishwa

                        Revina Pius akipokea baraka baada ya kuvalishwa KOFIA

                                             Sehemu ya WAZAMIVU katika Sheria

                  Zamakhishary Yassy akimvika ua Revina Pius baada ya kutunukiwa Shahada.

            Revina Pius akiwa na Alice mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili katika chuo kikuu cha Iringa

            Manyus Chaula, Mhasibu katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa akimpongeza Revina Pius

                                REVINA PIUS nje ya jengo jipya la Maktaba ya RUCO

                            REVINA PIUS nje ya jengo jipya la Maktaba ya RUCO

                                 Mchungaji Mwaikali akifurahia jambo na Revina

                                                Zamakhishary na Revina katika pozi

                                                     Revina na Edwin katika pozi


                                         Edwin na shemeji yake pamoja na Harrison

                                                 Harrison akimvalisha ua Revina

                            Zamakhisharyakimvika KOFIS YA SHAHADA Revina


                                                               Revina na Gondwe


 Revina Pius akivalishwa KOFIA na Mkuu wa Chuo cha Ruaha Mhashamu Baba Askofu  Tarcisius Ngalalekumtwa katika Mahafali ya 6 ya Chuo Kikuu cha Ruaha












Wednesday, November 27, 2013

DUNIA AFARIKI DUNIA



 Mhariri Mwandamizi wa magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Dunia Mzobora, amefariki dunia.
Mzobora (49) alifariki dunia ghafla jana saa 12 asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), alikokuwa amepelekwa kwa matibabu zaidi akitokea kwenye Hospitali ya Aga Khan, pia ya Dar es Salaam.

 
                                   Marehemu Dunia Mzobora
 
 Mussa, mdogo wa marehemu, alisema jana kuwa Mzobora alianza kujisikia vibaya juzi usiku akiwa nyumbani kwake, Tabata Mawenzi, na kupelekwa Aga Khan lakini hali ilizidi kuwa mbaya na ndipo alipopelekwa Muhimbili. Alifariki muda mfupi baadaye wakati madaktari wakiwa katika harakati za kuokoa maisha yake.

Mzobora ambaye hadi anafariki dunia alikuwa Naibu Msanifu Mkuu wa Uhuru, alifanya kazi hadi kumalizika kwa gazeti la Uhuru toleo la jana, akikaimu nafasi ya msanifu mkuu, akiwa buheri wa afya.

Taarifa zilizopatikana jana kutoka kwa ndugu wa familia zilisema maziko ya marehemu yatafanyika leo jijini Dar es Salaam.

Mzobora ambaye alizaliwa Aprili 6, 1964 Mwandiga mkoani Kigoma, alijiunga na Uhuru Publications Limited mwaka 1989 akiwa mwandishi wa habari mwanafunzi, baada ya kumaliza masomo ya ualimu ngazi ya cheti kutoka chuo cha Kasulu, mkoani Kigoma.

Kutokana na uwezo wake na kujituma kazini, mwaka uliofuata alithibitishwa kazini na kupandishwa cheo kuwa mwandishi kamili wa habari.

Mwaka 1992, alipandishwa cheo na kuwa msanifu kurasa wa Mzalendo na Burudani chini ya Msanifu Mkuu wa magazeti hayo kwa wakati huo, Hamisi Mkwinda, kabla ya kupandishwa na kuwa mwandishi wa habari daraja la pili mwaka 1994.

Mwaka 1995 alijiunga na kilichokuwa Chuo cha Uandishi wa habari cha Nyegezi (sasa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine), Mwanza na kuhitimu stashahada ya juu ya uandishi wa habari mwaka 1998.

Baada ya kurejea kazini, alipandishwa vyeo ngazi mbalimbali kuanzia mwandishi mwandamizi daraja la pili na hadi kufariki dunia kwake alikuwa Mhariri Daraja la Pili.
Miongoni mwa nyadhifa alizoshika ni pamoja na Kaimu Msanifu Mkuu wa Uhuru, Kaimu Mhariri wa Mzalendo na Kaimu Mhariri wa Makala.

Kutokana na kiu yake ya kupenda elimu, mwaka 2006 Mzobora alijiunga tena na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Mwanza kwa masomo ya shahada ya uzamili katika Mawasiliano ya Umma na uandishi wa habari.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema paponi. Amina.