Ajali za
barabarani zimeendelea kupoteza maisha ya wananchi ambapo zaidi ya abiria 4,500
wamefariki na wengine wakipata ulemavu wa kudumu nchini.
Akihutubia
wananchi katika Manispaa ya Iringa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt.
Emmanuel Nchimbi aliyemuwakilisha Rais katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki
ya nenda kwa usalama barabarani yanayofanyika kitaifa mkoani Iringa, amesema
kuwa takwimu za ajali zinazotolewa na
jeshi la polisi zinaonesha kuwa kwa karibu miaka mitano kuanzia mwaka 2008 hadi
Juni, 2012 vifo vya abilia vimefikia 4,532 wakati vifo vya watembea kwa miguu
vilivyotokana na ajali za barabarani vilifikia 5,117. Ameseam kuwa vifo vya
wapanda pikipiki ni 2,414 wakati wapanda baiskeli ni 2,171.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi
(kulia) alipotembelea banda la Jeshi la Polisi katika Maonesho ya wiki ya Nenda
kwa Usalama Barabarari yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Samora Manispaa
ya Iringa.
Picha ya pamoja ya wadau wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Emmanuel Nchimbi (wanne kulia waliokaa)
na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma (wa tano kulia waliokaa)
katika uwanja wa Samora Manispaa ya Iringa.
Amesema kuwa
madareva wa magari na pikipiki wamekuwa ni sehemu Kubwa ya vyanzo vya ajali
kutokana na kutokuzingatia mambo mbalimbali. Ameyataja mambo hayo kuwa ni
kuendesha kwa mwendo kasi usioruhusiwa kisheria na kuyapita magari yaliyopo
mbele bila ya kuchukua tahadhari. Mambo mengine ameyataja kuwa ni kutokuheshimu
alama na ishara za barabarani na kuendesha magari mabovu. Amesema mambo mengine
ni kwa wapanda pikipiki kutokuvaa kofia ngumu na kuendesha gari au pikipiki
bila leseni.
Nae Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Usalama barabarani, Pereira Silima amewataka wananchi
kuwa na muamko mkubwa katika kutembelea mabanda katika maonesho yanayoendelea
katika uwanja wa Samora ya Wiki ya nenda kwa usalama barabarani ili kuweza
kujifunza na kuuliza maswali juu ya masuala yote yanayohusiana na Wiki ya nenda
kwa usalama barabarani.
Akiongelea
mikakati ya kupunguza ajali za barabarani, Silima ameitaja kuwa ni pamoja na
askari kutoe elimu juu ya usalama barabarani katika shule za msingi na
sekondari ili kuwajengea wananfunzi uelewa mkubwa juu na dhana nzima ya usalama
barabarani. Amesema kuwa kila anayeomba leseni ya udereva ni lazima awe
amesomea udereva huo katika chuo kinachotambulika na serikali. Mkakati mwingine
ameutaja kuwa ni kuhakikisha kuwa mabasi ya masafa marefu yanakuwa na madereva wawili ili kusaidiana katika kazi
hiyo. Amesema mkakati mwingine ni kuwashirikisha wananchi katika Kutoa taarifa
mbalimbali dhidi ya watu wanaovunja taratibu za usalama barabarani ili waweze
kuchukuliwa hatua mapema kabla ya kusababisha maafa.
Nae Mkuu wa
Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika salamu zake amesema kuwa Mkoa
wa Iringa una mtandao wa jumla ya kilometa 8,051.20 za barabara. Amesema
mtandao huo ni chachu na kichocheo kikubwa cha maendeleo katika mkoa huo.
Amesema kuwa vyombo vya dola vinafanya kazi ya kuhakikisha usalama barabarani
unaimarishwa ili wananchi waweze kutumia barabara hizo vizuri kwa lengo la
kujiletea maendeleo.
Dkt. Christine
amesema kuwa hivi karibuni Serikali imefanikiwa kufanya matengenezo makubwa ya
barabara ta Tanzam kwa urefu wa kilometa 150 kwa gharama ya shilingi bilioni
127.7. amesema matengenezo hayo yameleta matokeo ya kupungua kwa gharama ya
usafirishaji kwa kupunguza uharibifu wa magari kutokana na mashimo yaliyokuwepo
awali.
Ámesema kuwa
changamoto Kubwa ni ajali barabarani kutokana na kuboreshwa kwa barabara kwa
sababu magari hienda kasi zaidi. Amesema pamoja na changamoto hiyo wadau wote
wakijipanga vizuri inaweza kukabiliwa.
Maadhimisho ya
Wiki ya nenda kwa usalama barabarani yanafanyika kitaifa mkoani Iringa na
yalianza kuadhimishwa nchini tokea mwaka 1994. Maadhimisho ya mwaka 2012
yanaongozwa na kaulimbiu isemayo ‘pambana na ajali za barabarani kwa vitendo,
zingatia sheria’ yatafikia kilele chake tarehe 22 Septemba, 2012 na maonesho
mbalimbali ya shughuli zinazoendana na Wiki hii yanaendelea katika uwanja wa
kumbukumbu ya Samora katika Manispaa ya Iringa
=30=
No comments:
Post a Comment