Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa akimkabidhi zawadi za IDD kutoka
kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania msimamizi wa Mahabusu ya watoto,
Bi. Ng’wanza John.
Wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60 wanaolelewa katika kituo cha serikali
cha kulea wazee kilichopo Mwanzange jijini Tanga wakifurahia zawadi za IDD zilizotolewa
na Rais Dkt. Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ametoa zawadi za Idd kwa vituo 12 vya watoto yatima na makundi maalumu nchini kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd El Haji.
Zawadi hizo zilikabidhiwa kwa vituo vya Msongola (Ilala), Dar Al Argram (Temeke), Furaha (Kinondoni), Makao ya wazee (Temeke), Makao ya Watoto ya Mother Thereasa (Kinondoni).
Vituo vingine ni Malaika kids Home (Mkuranga), Makazi ya wazee Kilima (Bukoba), Mahabusu ya watoto (Arusha), Mahabusu ya watoto (Tanga), Makazi yawazee Mwanzage (Tanga), Makao ya watoto Istikama (Pemba), Makazi ya wazee sebuleni (Unguja).
Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na mchele, mbuzi na mafuta ya kula vyote vikiwa na thamani ya Tshs. 5,505,000.
=30=
No comments:
Post a Comment