MZUNGUKO
wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara umekamilika leo baada ya Coastal
Union kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya maafande wa JKT Ruvu, kwenye uwanja
wa Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kipindi
cha kwanza kilianza kwa Wagosi kusuasua na kuwapa nafasi Ruvu kuutawala mchezo
ambapo ndani ya dakika ya kwanz awalikosa bao na kupata kona.
Hali
iliendelea hivyo kwa wachezaji wa Wagosi kupoteza mwelekeo ambapo katika dakika
ya tisa Ruvu walikosa bao la wazi baada ya beki
Wagosi Juma Nyoso alichelewa kufika baada ya Ruvu kupiga krosi na
mchezaji wao kuingia nao lakini golikipa wa Wagosi Shaaban Kado alikuwa makini
langoni.
Ilipofika
dakika ya 34 Ruvu waligongeana pasi ndani ya box la Wagosi, ambapo kutokana na
walinzi kukosa umakini Bakari Kondo wa Ruvu aliipatia bao la kuongoza timu
yake.
baada
ya hali kuwa hivyo kocha Joseph Lazaro wa Wagosi alifanya mabadiliko na kuwatoa
Hamad aliyeumia na kumuingiza Marcus Ndeheli. Halafu akamtoa Othman Tamim na
kumuingiza Abdi Banda.
Aidha
timu zilienda mapumziko Ruvu JKT wakiwa mbele kwa bao moja.
Kipindi
cha pili, mchezo ulianza kwa Coastal Union
kutawala uwanja, na kuonyesha nguvu ya kutaka kukomboa bao
lililopatikana kipindi cha kwanza.
Baadaye
alitolewa Suleiman Kassim ‘Selembe’ na kuingia Daniel Lyanga. Lakini hakuna
kilichobadilika mpaka daika tisini.
Mwamuzi
wa leo Hasheem Abdallah kutoka Dar es Salaam, alimaliza mchezo akiwa anazomewa
na mashabiki wachache wa Coastal Union waliojitokeza leo wakimshutumu
kuchezesha hovyo.
Kwa
hali hiyo Coastal Union itaendelea kushikilia nafasi ya saba ikiwa na point 16.
@Habari
na picha kwa hisani ya mtandao wa Coastal Union
No comments:
Post a Comment