Na. Magdalena
Nkulu
Mkoa
wa Shinyanga ni kati ya mikoa sita ya kanda ya Ziwa inayoshiriki katika
kongamano la uwekezaji kanda ya ziwa litakalofanyika jijini Mwanza kuanzia
tarehe 13-16 Februari 2014.
Mkuu
wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Ally N.Rufunga ametoa taarifa hiyo Jumanne ya wiki hii
katika mkutano na waandishi wa Habari ofisini kwake.
Mhe.Rufunga
amesema, kongamano la uwekezaji kanda ya Ziwa ni mkutano ulioandaliwa kwa ajili
ya kutangaza fursa za uwekezaji na kuwashawishi wawekezaji wa ndani na nje ya
nchi kuwekeza katika mikoa ya kanda ya Ziwa ambayo ni
Mwanza,Shinyanga,Mara,Kagera,Geita na Simiyu.
Mkoa wa
Shinyanga unashiriki kwenye kongamano hilo kwa sababu ya kutangaza fursa
zilizopo katika mkoa ambazo ni
·
Mazingira mazuri yanayofaa kwa utalii na kilimo
·
Hali ya usalama na amani hivyo hali ya matukio ya uhalifu ni ndogo
·
Nguvu kazi ya kutosha
·
Uwepo wa taasisi mbalimbali za Elimu zinazotoa ujuzi tofauti
·
Miundombinu ya usafiri na usafirishaji kutokana na mkoa
kuunganishwa na mikoa mingine ndani na nje ya nchi kama Kenya, Uganda, Burundi,
Rwanda, na DRC.
Kutokana
na kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Shinyanga kupitia kongamano
hilo,serikali inatarajia mafanikio makubwa ya kiuchumi na kijamii.
Kupitia shughuli mbalimbali za uwekezaji
katika viwanda za uzalishaji bidhaa, biashara, vyuo na taasisi wananchi wa mkoa
wa Shinyanga na maeneo ya jirani wategemee kupata ajira, wataboresha na
kuongeza thamani ya mazao ya mifugo na kilimo ili kuzalisha malighafi na fursa
nyingi zitaongezeka.
Tayari
mkoa wa Shinyanga imekwisha anza kunufaika na shughuli za uwekezaji wa viwanda
ambavyo baadhi ya wawekezaji hasa wa nje ya nchi wamejenga na wameanza
uzalishaji kama kiwanda cha ngozi (Ibadakuli),kiwanda cha kutengeneza nyuzi
(Nhelegani),kiwanda cha mafuta ya kupikia (Nhelegani) na kiwanda cha mwekezaji
mzawa cha Maji na soda cha “Jambo Group of Companies”.
Kongamano
hili ni kutokana na mkakati wa serikali wa kukuza uchumi kupitia sekta ya
uwekezaji hivyo ni muhimu kutangaza fursa zilizopo ili kuwavutia zaidi
wawekezaji kuja katika mkoa wa Shinyanga.
Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga
No comments:
Post a Comment