Serikali
imezipongeza shule zisizo za serikali kwa kufanya vizuri katika matokeo ya
kitaifa kwa mitihani ya kuhitimu darasa la saba, kidato cha nne na sita kanda
ya Nyasa.
Gerald G. Guninita,
Kauli hiyo
imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dkt. Christine Ishengoma katika hotuba
yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita
katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Kalenga mjini Iringa.
Dkt. Ishengoma
amesema “niwapongeze sana kwa namna ya pekee kutokana na ukweli kwamba, ninyi
mmekuwa ni mfano bora wa malezi ya mtoto wa kike kwani mara nyingi wanafunzi
hufanya vizuri kitaifa katika matokeo ya mitihani ya kuhitimu darasa la saba,
kidato cha nne na cha sita. Shule zisizo za serikali zinaongoza katika kufanya
vizuri”. Amesema kwa matokeo haya inaonesha wazi mmejipanga vizuri kulisaidia
taifa kutoa elimu yenye manufaa na tija kwa watanzania.
Amesema
mafanikio hayo yanadhihirisha nia njema waliyonayo wamiliki wa shule binafsi katika
kulielimisha na kuliendeleza taifa. Amepongeza juhudi za kukutana na kujadili
na kupeana uzoefu na kubadilishana mbinu za ufundishaji katika kutoa elimu bora
kwa wanafunzi.
Mkuu wa Mkoa
amesema kuwa pamoja na kufanya vizuri kwa shule binafsi, zipo zinazofanya
vibaya pia kutokana na wanafunzi wengi kutohudhuria masomo kwa kukosa ada,
gharama kubwa ya masomo. Sababu nyingine amezitaja kuwa ni uhaba wa walimu kwa
baadhi ya masomo, uongozi mbaya na migogoro katika shule pamoja na mambo
mengine.
Akiongelea
mikakati ya kuboresha elimu itolewayo nchini, amesema kuwa serikali imeamua
kufanyia marekebisho sera ya elimu na mafunzo ya ufundi ya mwaka 1995. Amesema
kuwa tayari kuna mambo mengi ambayo yamerekebishwa kwa lengo la kuendana na
mahitaji ya utoaji wa elimu bora inayopatikana kwa wote.
Aidha, amewashauri
kujenga vyuo vya ualimu na vyuo vingine ili kukidhi hitaji kubwa la walimu
katika shule zote za serikali na binafsi na wataalamu wengine.
=30=
No comments:
Post a Comment