Mkoa
wa Iringa unaandika historia nyingine kesho ambapo maamuzi muhimu yatafanyika
kwa mustakabali wa Mkoa huu.
Maamuzi
hayo yanatarajia kufanyika katika kikao maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa
(RCC) kitakachofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo.
Kwa
mujibu wa Agenda zilizopatikana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa, ni
pamoja na:-
1.
Mapendekezo ya kugawa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo
2.
Mapendekezo ya kugawa Jimbo la Uchaguzi la Kilolo
3.
Mapendekezo ya kuanzisha Jimbo jipya la Uchaguzi la Mafinga
4.
Mapendekezo ya kugawana Mali na Madeni kati
ya
Halmashauriya Wilaya ya Mufindi na Mji wa Mafinga
5.
Mpango na Bajeti ya Mkoa wa Iringa kwa mwaka 2015/2016.
No comments:
Post a Comment