Christopher
Philemon - NJOMBE
Mamlaka
ya Maji Mkoa wa Njombe (NJUWASA)
imepokea kiasi cha fedha 2.6 ( 2,577,138,890.00) bilioni
kutoka Wizara ya Maji toka mwaka
2013 kwa ajili ya kuboresha hudumaya maji katika Mji wa Njombe.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Mkoa wa
Njombe Mhandisi, Daudi Majani amesema kuwa mpaka sasa fedha hizo zimetumika
kujenga chanzo cha maji cha Nyenga,matanti
matatu ya maji na utandazaji wa mabomba ya maji ambapo ujenzi wake unatarajiwa
kukamilika mwisho wa mwezi wa saba mwaka huu.
Alisema kuwa mpaka sasa Ujenzi wa
kidakio cha maji umekamilika na ujenzi
wa matanki matatu yaliyopo katika maeneo ya Airport, Kambalage, Igeleke na
Nzengelendete na kila tenki linauwezo wa
ujazo wa lita 135,000 kila mojaHatua inayoendelea sasa ni utandazaji wa mabomba
ya maji katika maeneo mbalimbali ya Mji wa Njombe.
Mradi huo ukikamilika utawezesha
kufanya mji wa Njombe kuongeza upatikanaji wa maji kutoka asilimia 55 hadi 80 na kufanya mji huo kuondoka na huwaba wa maji
.
Majani amesema hayo jana kwenye ziara
ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk. Rehema Nchimbi alipotembelea vyanzo vya maji na
kuangalia mtandao wa maji katika mji wa Njombe.
Mkuu huyo wa Mkoa amezitaka
Halmashuri za Mji wa Njombe kushirikiana na mamlaka ya maji Mkoa wa Njombe
kuakikisha wanatoa elimu kwa wananchi waliopo kwenye vyanzo vya maji ili
kutunza vyanzo vya hivyo.
=30=
No comments:
Post a Comment