Christopher Philemon -
NJOMBE
Zaidi ya wachina 6,000 wanatarajiwa kuingia katika Mkoa wa
Njombe kwenye sekta ya madini hasa makaa ya mawe na chuma kwenye eneo la Liganga na Mchuchuma
wilayani Ludewa.
Hayo yamesemwa jana kwenye Ukumbi wa Lutheran Makambako na
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dk. Rehema Nchimbi alipokuanaongea na watumishi wa
Halmashuri ya Mji Makambako, alisema kuwa Mradi wa Linganga na Mchuchuma unatarajiwa kuanza kuchimbwa
makaa ya m awe na chuma hivi karibuni utatoa ajira zaidi ya 30,000
zikiwepo za wazawa na wageni.
Kutokana na hilo amewataka watumishi
wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya Ardhi kuakikisha wanaweka mipango
mizuri ya matumizi ya ardhi na kupima viwanja ili kuwavutia wawekezaji
mbalimbali katika ujenzi wa Hoteli za kisasa na halmashuri kuakikisha
wanaboresha miundombinu ya Maji na barabara .
Dk. Nchimbi alisema kuwa mpaka sasa
shirika la maendeleo ya Taifa (NDC) limeanza mchakato wa uthamini wa mali za wananchi ili waweze kulipwa fidia
kupisha mradi huo.
Aliwataka wananchi wa Makambako na Njombe kwa Ujumla kujiandaa na
ujio wa wageni mbalimbali kwa kufuga kuku, ng’ombe pamoja na mifugo mingine ili
kuweza kuwauzia wageni hao na kuongeza
kipato cha familiya.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji
Makambako Hanana Chesco Mfikwa alisema kuwa
wanajiandaa kwa kuwapokea wageni hao kwa kuakikisha wanaweka mipango
mizuri ambayo itasaidia wageni kuwekeza zaidi katika eneo la Makambako.
=30=
No comments:
Post a Comment