Na
Mwandishi Maalum Mbeya
Jamii
imetakiwa kutumia chumvi yenye madini joto ili kujenga ukuaji wa akili na
kuepukana na ulemavu.
Kauli
hiyo litolewa na Afisa Lishe Manispaa ya Iringa, Anzael Msigwa alipokuwa
akifafanua umuhimu wa madini ya joto katika chumvi ya majumbani kwa wananchi
waliotembelea banda la maonesho la Manispaa ya Iringa lililopo katika uwanja wa
John Mwakangale jijini Mbeya.
Msigwa
alisema “madini joto ni madini ambayo
yanawekwa kwenye chumvi ili kuzuia ugonjwa wa tezi la shingo na kwa mama wajawazito
madini hayo yanazuia baadhi ya ulemavu wa viungo kwa watoto. Madini joto
yanasaidia ubongo wa mtoto akiwa tumboni kukua vizuri na kuzuia udumavu”.
Akiongelea
umuhimu wa madini joto mwilini, Msigwa alisema kuwa madini joto yanahitajika
kwa wingi wakati wa mabadiliko ya kimwili hasa kuvunja ungo, kubalehe na wakati
wa ujauzito. Faida nyingine ya madini hayo ni kusaidia ukuaji wa mtoto aliye
tumboni na ukuaji wa maendeleo yake baada ya kuzaliwa. Madini hayo pia husaidia
ukuaji wa mwili na akili.
Afisa
lishe huyo alisema kuwa kukosekana kwa madini joto mwilini, husababisha uvimbe
wa tezi la shingo, ugumu katika kuelewa na kufundishika na kudumaa mwili na
utaahira. Athari nyingine ni kuharibika kwa mimba na mtoto kuzaliwa akiwa na
uzito pungufu na mtoto kuzaliwa akiwa na ulemavu wa viungo.
Alishauri
kuwa chumvi inatakiwa kuhifadhiwa katika kasha kavu, lenye mfuniko na
kuhifadhiwa mbali na joto.
Alisema
kuwa kwa mujibu wa sheria ya chumvi ya mwaka 2010, inatoa idhini kwa maafisa
wenye dhamana kukagua chumvi sehemu za kuhifadhi na kuuza chumvi.
=30=
No comments:
Post a Comment