Na
Mwandishi Maalum Mbeya
Wateja
wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Mbeya wametakiwa kuwa
walinzi wa miundombinu ya maji ili idumu na kuwanufaisha kwa muda mrefu zaidi.
Kauli
hiyo ilitolewa na Afisa huduma kwa wateja wa Mamlaka ya majisafi na usafi wa
mazingira mjini Mbeya, Hilda Nzary alipokuwa akielezea umuhimu wa mkataba
wa huduma kwa mteja wa mamlaka hiyo katika viwanja vya Nanenane jijini Mbeya.
Afisa Huduma kwa Wateja, Hilda Nzary |
Nzary alisema “kwa mujibu wa mkataba wa huduma kwa mteja, wajibu wa mteja ni kuzuia
wizi, uharibifu mchepusho wa mita na vitendo vya rushwa ikiwa watumishi wa
mamlaka wameomba”.
Aliongeza kuwa mteja anawajibu wa kutoa taarifa kwa
uongozi wa mamlaka juu ya vitendo vyovyote vinavyohatarisha usafi na usalama wa
maji ili huduma hiyo iendelee kuwa salama kwa jamii nzima na kuwa endelevu.
Mteja pia anawajibu wa kulipia huduma ya majisafi na majitaka na kutunza dira
ya maji inayopima wingi wa maji yanayotumika.
Afisa
huduma kwa wateja alisema kuwa, kwa wateja kutimiza wajibu huo, watarajie
huduma bora ya uhakika na yenye ufanisi wa hali ya juu katika muda mfupi na
kurejeshewa huduma ya maji katika muda usiozidi saa 24 baada ya kulipia ankara
yake yote. Aliongeza kuwa mteja anayo haki ya kutoa taarifa kwa maandishi iwapo
haridhiki na huduma anazopata.
Akiongelea
ubora wa huduma zitolewazo na mamlaka hiyo, alisema kuwa mamlaka hiyo
itahakikisha inaendelea kuimarisha viwango vya ubora wa huduma zinazotolewa kwa
kupitia hali ya utendaji kila baada ya miezi mitatu. Mamlaka imeweka mtandao wa
kukusanya habari kutoka kwa wateja wa ndani na wateja wa nje ili iweze kupata
taarifa sahihi zitakazoisaidia kufanya maamuzi sahihi ya kuboresha huduma kwa
wateja.
Mamlaka
ya majisafi na usafi wa mazingira mjini Mbeya ilianzishwa mwaka 1998 kwa Sheria
namba 8 ya Maji, ya mwaka 1997 kifungu 3(1) ikiwa inahudumia wateja 48,000.
=30=
No comments:
Post a Comment