Na
Mwandishi Maalum Mbeya
Mkuu
wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika ameitaka benki ya kibiashara ya Akiba (Akiba Commercial
Bank) kujitangaza zaidi katika vyombo vya habari ili iweze kufahamika zaidi kwa
wananchi.
Ushauri
huyo aliutoa alipotembelea benki hiyo katika viwanja vya John Mwakangale katika
maonesho ya Nanenane jijini Mbeya.
Ntinika
alisema kuwa ili benki hiyo na huduma zake ziweze kufahamika zaidi kwa wananchi
lazima benki hiyo itengeneze mkakati wa kujitangaza kwa wananchi kupitia vyombo
vya habari. “Pamoja na huduma nzuri mnazozitoa lakini kama hamjitangazi si
rahisi kwa wananchi kuwafahamu na kufahamu huduma zenu. Tumieni fursa hii ya
maonesho ya kilimo Nanenane kujitanga zaidi na hasa kutangaza mipango yenu ya
kumnufaisha mkulima pamoja na mambo mengine” alisema Ntinika.
Ntinika
ambaye pia ni mtaalam mbobezi katika masuala ya fedha na ukaguzi wa mahesabu,
alisema kuwa wananchi wengi hawana uelewa wa masuala ya kibenki hivyo kukosa
huduma na fursa nyingi zinazopatikana kupitia taasisi za kifedha. Aliitaka
benki hiyo kupanua wigo wake wa huduma ili kuwanufaisha wananchi wengi wa
wilaya ya Mbeya.
Nae
Afisa mikopo wa benki ya kibiashara ya Akiba, Anthony Kunambi alisema kuwa
benki yake inalenga wajasiliamali wadogo na wa kati kwa kuwapa elimu ya
ujasiliamali ili waweze kufanya kazi zao kwa tija na faida zaidi. Alisema kuwa
miongoni mwa huduma wanazotoa ni pamoja na akaunti za amana, hundi, akaunti
maalumu ya wafanyabiashara na huduma za kuwaleta karibu Vicoba na taasisi za
kifedha na kuwaelimisha umuhimu wa Vicoba kutumia huduma za kibenki badala ya
mfumo wa awali wa kujiwekea akiba majumbani.
Akiongelea
jinsi benki yake inavyojishughulisha na kilimo, Kunambi alisema kuwa benki hiyo
imekuwa ikitoa huduma ya mikopo kwa wakulima na wafugaji.
“Kwa mkoa wa Mbeya tumekuwa tukitoa mikopo kwa wafugaji wanaofuga kisasa
lakini katika mkoa wa Arusha tumekuwa tukifanya kazi na wafugaji wanaofuga
kizamani. Katika mkoa wa Arusha tumekuwa tukifadhili mradi wa kunenepesha
ng’ombe na wanyama wamekuwa wakikatiwa bima ili kumhakikishia mfugaji uhakika
kwa mifugo yake endapo janga litatokea”.
Sabina
Stanley ambaye ni msimamizi wa mikopo wa benki hiyo tawi la Mbeya, alisema kuwa
benki hiyo imaendelea na mradi wa majaribio katika sekta ya kilimo kwa kuanza
na miradi michache katika mikoa ya Mbeya, Arusha na Dodoma. Alisema kuwa benki
yake ilitoa mikopo kwa wakulima wa Litenga zaidi ya shilingi bilioni moja kwa
vikundi 39 vya wakulima mwaka 2015. Nyingine ni mashine ya kukaushia kahawa
yenye thamani ya dola za mimarekani 200 na kampuni ya Rogimwa iliyokopeshwa
milioni 200.
Benki
ya kibiashara ya Akiba (ACB) ina jumla ya matawi 18 kati ya matawi hayo, 13
yapo mkoani Dar es Salaam, wakati mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro
na Dodoma ikiwa na tawi mojamoja.
=30=
No comments:
Post a Comment