Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa- Iringa
Kamati
ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa imehakikishiwa kufanya kazi kwa amani
na usalama mkoani Iringa kutokana na vyombo vya usalama kuwa macho muda wote.
Uhakika
huo ulitolewa na mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mkoa wa Iringa,
Amina Masenza alipokuwa akiongea na kamati ya Bunge ya utawala na serikali za
mitaa katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa Mkoa, kamati hiyo ilipofanya ziara
mkoani hapa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Amina Masenza (kusho), kulia ni Mwanne Mchemba, Makamu Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa |
Masenza
ambaye pia ni mkuu wa Mkoa wa Iringa alisema kuwa Mkoa wa Iringa upo shwari.
Hali ya usalama ni nzuri kuiwezesha kamati hiyo kufanya ziara ya kikazi katika
hali ya usalama na utulivu. Aidha, aliongeza kuwa wananchi mkoani Iringa
wanajitambua katika kutekeleza majukumu yao.
“Wananchi mkoani Iringa hasa wakulima katika msimu huu wa kilimo
wanajitambua na hawashurutishwi kutekeleza majukumu yao ya kilimo” alisema
Masenza.
Wakati
huohuo, makamu mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa, Mwanne
Mchemba alisema kuwa dhumuni la ziara ya kamati yake ni kukagua miradi ya
maendeleo wilayani Kilolo kwa fedha zilizotolewa na serikali mwaka 2016/2017.
“Tunajua kuwa mkuu wa Mkoa ni jembe katika
usimamizi wa uhamasishajai wa maendeleo. Hivyo, kamati inataka kujiridhisha na
matumizi ya fedha za serikalai hasa thamani ya fedha kabla ya serikali kuidhinisha
fedha nyingine kwa Wilaya ya Kilolo” alisema Mchemba.
=30=
No comments:
Post a Comment