Na. Ofisi ya Mkuu wa Mkoa-Iringa
Kamati
ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa imepongeza ushirikiano baina ya
serikali na chama tawala wilayani Kilolo kwa maendeleo ya wananchi.
Pongezi
hizo zilitolewa na mjumbe wa kamati ya Bunge ya utawala na serikali za mitaa, Magreth
Sitta katika ukumbi wa halmashauri ya Wilaya ya Kilolo wakati kamati hiyo
ilipotembelea mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Kilolo hivi karibuni.
Sitta
ambaye ni mbunge wa Urambo alisema kuwa mshikamano baina ya serikali na chama
tawala ni muhimu katika kufanikisha dhamira ya serikali ya kuwaletea maendeleo
wananchi. Alisema ili mchakato wa maendeleo uende vizuri ni muhimu kwa serikali
na chama tawala kuzungumza lugha moja. Chama tawala kinawajibu wa kuisimamia
serikali katika utekelezaji wa Ilani ya chama.
=30=
No comments:
Post a Comment